Jamhuri Kiwello 'Julio' ana vituko kweli. Licha ya kupokea
kipigo cha mabao 8-0 kutoka kwa Yanga jana, Kocha huyo
mkuu wa Coastal Union amewaacha watu huo baada ya
kusema kuwa alitarajia kufungwa.
Julio ambaye yupo kwenye mkataba wa kuifundisha Coastal
Union kwa mkopo, amesema kuwa alitambua mapema kuwa
timu yake itafungwa na Yanga kutokana na kupewa taarifa
kwa kushtukizwa kuwa wanatakiwa waje Dar kucheza na
Yanga igawa wao hawakujiandaa na hilo.
"Nilitarajia kufungwa ingawa sio kwa idadi kubwa ya magoli
kama haya ya leo. Tulishtukizwa tukiwa kwenye bonanza
tukaambiwa tunatakiwa kucheza na Yanga. Sisi kwa kweli
hatukujiandaa kikamilifu kwa ajili ya mechi ya Yanga ila
hatukuwa na jinsi ya kukataa kucheza," alilalama Julio.
Kipigo hiko kutoka kwa Yanga huenda kikamweka kikaangoni
Julio ambaye alipewa jukumu la kuinoa Coastal kwa muda
chini ya kocha James Nandwa ambaye muda mfupi baada ya
Julio kutua, alitimka nchini kwao Kenya akidai kutofurashwa
na ujio wake klabuni hapo.
Julio atapatapa
Info Post