Mbaya wa Liverpool aipa ushindi Man u
Info Post
Mchambuzi mahiri wa soka wa kituo cha televisheni cha Skysports cha Uingereza, ameitabiria timu ya Manchester United kuibuka na pointi tatu katika mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Manchester City utakaopigwa Jumapili hii kwenye uwanja wa Old Trafford.
Merson ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alijizolea umaarufu baada ya kutabili kuwa Arsenal itaipa kipigo Liverpool kwenye mchezo uliozikutanisha timu hizo Jumamosi iliyopita jambo ambalo lilitokea kwa Arsenal kuibuka na ushindi mnono wa bao 4-1.
Na safari hii Mersdon ametabiri kuwa Manchester City haitofua dafu mbele ya United kutokana na ubora wa City kupungua katika siku za hivi karibuni huku United wakionekana kuimarika.
"Ungeniuliza kipindi cha wiki sita nyuma, bila shaka yoyote ningeipa nafasi City kuwa washindi lakini kwa sasa Manchester United nadhani ndio chaguo langu kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo kwani wamebadilika kwa kiasi kikubwa dakika hizi za mwisho," alisema Merson.
Alisema kuwa kikubwa kitakachoiangusha Manchester City ni kushuka kwa hali yao ya kujiamini kunakotokana na kufanya vibaya kwenye mechi zake za hivi karibuni.