Kocha wa Yanga Hans Pluijm, amewataka wachezaji wa timu hiyo kutuliza akili pindi watakapokutana na timu ya Etoile Du Sahel Jumamosi.
Pluijm aliyaongea hayo jijini jana wakati alipozungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya timu yake kuelekea pambano hilo la raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
Pluijm alisema kuwa Etoile ni timu ya kawaida kama zingine ambazo wamewahi kukutana nazo na kikubwa kitakachowasaidia wachezaji wa timu yake kuibuka na ushindi dhidi yao ni utulivu wa akili na kutowahofia Waarabu hao.
"Tumewaandaa wachezaji wetu kisaikolojia na nimewaambia kuwa huu ndio wakati wao kujitangaza kimataifa kwani Dunia nzima itakuwa inawatazama. Tumejiandaa vyema kuwakabili Etoile na tuna imani Mungu akitusaidia tutaibuka na ushindi," alisema Pluijm.
Wakati huohuo Etoile inatarajia kuwasili jijini usiku wa kuamkia leo mnamo mida ya saa 8.
Pluijm ataja mbinu ya kuwaua Waarabu
Info Post