Kocha Mkuu wa Mbeya City Juma Mwambusi, amesema
kuwa atahakikisha timu yake inaibuka na ushindi kwenye mechi
tano za Ligi Kuu zilizobaki ili wamalize ligi wakiwa kwenye
nafasi nzuri.
Mbeya City inayoshika nafasi ya saba kwenye msimamo wa
ligi hiyo, ni miongoni mwa timu zilizo kwenye hatari ya kushuka
daraja kutokana na kuwa na tofauti ya pointi chache kati yao
na timu zilizo mkiani mwa ligi.
Akizungumza na Mwandishi wetu jana, Mwambusi alisema
kuwa mkakati wao kwa sasa ni kushinda mechi zao tano
zilizobakia ili kutimiza malengo waliyojiwekea mwanzoni mwa
msimu.
"Tuliweka malengo ya kumaliza ligi tukiwa kwenye nafasi nne
za juu kama tulivyofanya msimu uliopita. Mwanzoni
hatukuanza vizuri ila kwa sasa naweza kusema kuwa tumerudi
kwenye mstari na tunataka kumaliza ligi vizuri," alisema
Mwambusi.
Mwambusi aliongeza kuwa licha ya timu yake kukumbwa na
jinamizi la majeruhi sambamba na beki wake Juma Nyosso
kufungiwa mechi nane, bado timu hiyo imeweza kusimama
imara na kuondoa hali ya kufanya vibaya mara kwa
iliyowakuta mwanzoni mwa msimu.
Sare ya Azam yampa kiburi Mwambusi
Info Post