Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya soka ya wanawake 'Twiga Stars' Rogasian Kaijage ameliomba Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuitafutia mechi za kirafiki timu hiyo ili ifanye vyema kwenye michezo ya Afrika,
Kauli ya Kaijage imekuja siku chache baada ya Twiga Stars kufanikiwa kufuzu kwenye michezo ya Afrika, licha ya kupokea kipigo cha bao 3-2 kutoka kwa Zambia huku yenyewe ikifuzu kwa faida ya bao la ugenini.
Akizungumzia mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo huo, Kaijage alisema kuwa Twiga Stars haikucheza mechi nyingi za kirafiki kuelekea kwnye mechi hiyo jambo ambalo liliwagharimu.
Alisema kuwa sasa timu hiyo inatakiwa iandaliwe mapema kwa kupewa mechi za kirafiki hasa na timu zenye uzoefu ili waende kushindana kikamilifu kwenye mashindano hayo yatakayofanyika mwezi Septemba mwaka huu.
Katika mchezo wa marudiano dhidi ya Zambia, Twiga walionekana kuchoka jambo lililowapa mwanya wapinzani wao kutawala mechi hiyo na kuibuka na ushindi.
Twiga Stars walilia mechi za kirafiki
Info Post