Breaking News
Loading...
Saturday, 19 May 2018

Info Post

Antonio Conte amefanikiwa kumtungua Jose Mourinho na kuipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United na kutwaa taji la kombe la FA dimba la Wembley.

Goli pekee la Mbeligiji Eden Hazard kwa mkwaju wa penati kipindi cha kwanza limetosha kuipa Chelsea ubingwa wa FA msimu wa 2017/2018.

Baada ya msimu wake wa kwanza kutwaa mataji mawili ya Europa na EFL , msimu huu Jose Mourinho katoka ‘ kapa ‘ bila taji lolote, mafanikio pekee ni ya kufuzu kucheza ligi ya mabingwa Ulaya.