Breaking News
Loading...
Thursday, 24 May 2018

Info Post
Unalifahamu Dimba la NSC Olimpiyskiy-Kyiv. ?? Ikiwa zimebakia siku mbili kuelekea mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya maharufu kama "UEFA CHAMPIONS LEAGUE "Mchezo utakao chezwa Nchini Ukraine ukiwakutanisha Miamba ya Hisapani Real Madrid dhidi Liverpool wikiendi hii Leo hii nimelenga hasa kukufahamisha Dimba ambalo fainali hizo za ligi ya Mabingwa zitafanyika msimu huu 2017/18 na linapatikana wapi?

Kyiv ndiyo Mji mkuu wa Nchi ya Ukraine, ni mji uliopo katikati ya Ukraine ukiwa na hali ya ujoto ujoto katika kipindi cha Machipuko ( Spring ) na kipindi cha kiangazi (Summer)ukiwa na Bichi kibao za kutosha takribani Kilomita 2,000 hivi kutoka London na Paris, na ni umbali sawa na kutoka  New York na  Shanghai. 
Baada ya Kuijui Ukraine hususani Kyiv sasa nikupeleke moja kwa moja katika dimba la Olimpiyskiy au "NSC Olimpiyskiy Stadium". Chimbuko la uwanja huu ifahamike kuwa ulijengwa Kwa ajili ya tamasha la kimataifa la michezo lililokuwa likidhaminiwa na umoja wa Kisoviet likijulikana kama "Spartakiade" na ulifunguliwa rasmi Agosti 12, 1923 na kufanyiwa marekenisho mara kadha huku mwonekano huu wa sasa ni matengenezo yaliyofanyika mwaka 2012 kwa ajili ya mashindano ya "UEFA EURO 2012," ambapo michezo mitano ikiwemo fainali ilichezwa katika dimba hilo. • Tangu kipindi hicho uwanja huu umekuwa ukitumika kama dimba la nyumbani la timu ya taifa ya 
Ukraine, pia klabu ya FC Dynamo Kyiv  imekuwa ikitumia uwanja huu kwa michezo ya Mabingwa barani Ulaya  kama dimba lao la nyumbani. • Herufi NSC ambazo zipo kabla ya jina la uwanja yaani 'NSC' Olimpiyskiy Stadium linamaana ya (National Sports Complex). Uwanja mkubwa wa Taifa wa Michezo. • Aidha Kubwa zaidi ambalo ungetaka kujua ni idadi ya watu ambao dimba hili uchukua, na hapa ndiyo pahala sahihi pa kuweza kufahamu hilo , ebwana uwanja huu unachukua watu 70,050.Tusubiri kuona ni mashabiki wa timu gani wataujaza sana uwanja huo siku ya Jumamosi???