Radja Nainggolan ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa baada ya kutemwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ubeligiji kuelekea fainali za kombe la Dunia, Urusi.
Radja Nainggolan kiungo wa Roma hakujumuishwa kikosini na kocha Roberto Martinez katika kikosi chake cha awali cha Ubeligiji huku akicheza mechi mbili tu katika hatua ya kufuzu ndani ya Ubeligiji.
Radja Nainggolan mwenye umri wa miaka 30, amefanikiwa kucheza mechi 29 za timu ya taifa ameandikia kupitia ukurasa wake wa Instagram.
. " Kwa tabu sana maisha yangu ya soka la kimataifa yamefika mwisho . Mara zote nimekuwa nikifanya kila kitu kuwakilisha taifa langu. Muda mwingine kuwa wewe kama wewe inasumbua . Kuanzia siku ya leo nitakuwa mshabiki wa kwanza."