Juma K Juma, kamwagia ‘ kitumbua’ Mchanga
Kwa mara nyingine tena golikipa Juma Kaseja kaonyesha uwezo wake wa kucheza mkwaju wa penati baada ya kudaka penati ya Emmanuel Okwi na kuisaidia Kagera kuitungua Simba SC kwa 1-0 .
Harakati za Simba SC kumaliza msimu bila kufungwa zimefikia kikomo leo hii katika siku ambayo wanakabidhiwa kombe la ubingwa wa VPL 2017/2018.
Mtanange wa leo ulikuwa ukishuhudiwa na Rais wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.