BONANZA LA WAKONGWE
Info Post
Lile bonanza la wakongwe linaloshirikisha timu na wachezaji waliocheza ligi daraja la kwanza leo Vodacom linategemea kutimua vumbi mwisho wa mwezi huu wa nane katika viwanja vya sigara TCC,mtifuano huo utashirikisha timu za Yanga ,Simba,Sigara,Plisner,Milambo ya Tabora ,Bandari,Reli Morogoro,Ushirika Moshi,,Coastal ya Tanga na Tanzania Stars kama wageni waalikwa.
Wadau wa michezo tunaomba mtusaidie kati ka hali na mali ili kufanikisha Bonanza hilo ambalo hadi sasa halina mdhamini yeyote ingawa linakutanisha majina mengi makubwa yaliyowika zamani kama vile Mohamedy Mwameja,Sunday Manara,Edibilly Lunyamila,Ally Mayai,George Masatu,Yusufu Macho,Ngade Chabanga,Musrafa Hoza na waliopita kama tofauti na yanga na simba ,Mtono,Madundo,Abuu Napili,Abdul Kipenga,Kaunda mwakitope na wengine weengi
Gharama za kuwakutanisha wakongwe hao ambao wengi wao kwa sasa vipato vyao ni vya kawaida sana lakini wamefanya mambo mengi ya kuenziwa ni kama vile gharama za uwanja,kulipa waamuzi,kulipa muziki kwa ajili ya kuburudisha watazamaji ikiwa ni pamoja na kutangaza,maji ya kunywa wakati wa mchezo ili kupooza makoo ya wakongwe hao,kupata chakula baada ya mchezo na kutoa zawadi mbalimbali kwa ajili ya washindi.
Mara nyingi kutoa ni moyo na tunawakaribisha wote wenye kuwajali wakongwe hao kwa chochote na sisi kama waandaaji hatutasita kutoa shukrani zetu hadharani kwa kuonesha mfano kwa chochote utakachoona kinafaa na yote kwa yote mnakaribishwa sana siku hiyo ya tarehe 31 kuanzia saa 2 asubuhi kujionea wakongwe walikuwa wanafanya nini enzi hizoo
kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Mratibu wa bonanza hilo Kenny Mwaisabula Mzazi 0652875794