Breaking News
Loading...
Monday, 29 September 2014

Info Post


Klabu ya Liverpool inapanga kuanza haraka mazungumzo ya kumuongezea na kumboreshea mkataba nyota wake Raheem Sterling  ambaye ameanza kuwindwa na klabu ya Real Madrid ya Hispania.

Kutoka kambi ya klabu hiyo ya Merseyside habari zinasema Sterling (19) ambaye bado ana mkataba na Liverpool mpaka mwaka 2017 huku akipokea mshahara wa paundi
30,000 kwa juma ameandaliwa maboresho makubwa yatakayomfanya avune zaidi ya paundi 100,000 ili aendelee kukipiga Anfield kwa miaka mingine mingi.
Sterling ni kati ya nyota bora na tegemeo katika kikosi cha Brendan Rodgers msimu huu hasa baada ya kuondoka kwa mshambuliaji Louis Suarez aliyetimkia klabu ya Barcelona ili kumfanya atulize akili yake klabuni hapo mkataba mnono uko mezani kwa ajili yake.