Breaking News
Loading...
Monday, 29 September 2014

Info Post

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya liverpool ambaye sasa anakipiga kwenye timu ya stoke city peter crouch  usiku wa jana aliifungia timu yake ya stoke city bao pekee la mchezo kwa kichwa maridadi baada ya kuunganisha mpira uliopigwa na victor mosses dakika ya 15 ya mchezo.

bao ilo la peter crouch limemuweka kwenye hali mbaya kocha wa newcastle allan pardew.

 Newcastle united inayokamata nafasi ya 19 mpaka sasa haijashinda mchezo hata mmoja wa ligi kuu baada ya kutoa sare mechi tatu na kufungwa mechi 3 katika michezo 6 waliyocheza mpaka sasa .

Washabiki wa newcastle usiku wa jana waliingia uwanjani na mabango ya kumhamasisha bosi wa newcatle united Mike Ashley amtimue kocha pardew.


Huu ni mwanzo mbaya wa ligi kwa newcastle,mara ya mwisho kuanza ligi vibaya kama msimu huu ni miaka 11 iliyopita