Ukiniuliza
kiungo bora Duniani niliyewai kumshuhudia akicheza mpira sitasita kumtaja Frank
Lampard.Kiungo mwenye nguvu,stamina ya kutosha,Pasi za uhakika bila kuusahau
mguu wake ambao ni rafiki wa nyavu.Frank lampard ni kiungo aliyefunga magoli
mengi kwenye historia ya soka.Ameifungia Chelsea magoli zaidi ya 200,Kwenye
ngazi ya klabu hakuna alichokibakiza baada ya kushinda karibu kila kombe akiwa
na Chelsea.
Huyo ndio
Super Frank Lampard,Kiungo mwenye sura mbili.Sura ya kwanza akiwa na timu za
vilabu na sura ya pili akiwa kwenye timu ya Taifa ya Uingereza.Alipokua
akiitumikia Chelsea alikua roho ya Chelsea,siku asipokuwepo frank lampard lazima utagundua udhaifu wa Chelsea.Mafanikio
yake ya kuwa mchezaji bora wa Dunia na Mchezaji bora wa ulaya nyuma ya
Ronaldiho mwaka 2005 yote aliyapata akiwa kwenye sura yake ya kwanza na Chelsea.
Lakini Frank Lampard yule yule wa Chelsea anakuwa tofauti na lampard wa Timu ya
Taifa ya uingereza.Lampard wa uingereza amefeli.Ameshindwa kuwapa waingereza
kile walichokiona anawapa Chelsea.Mpaka mwaka huu anastaafu kuchezea timu ya
taifa hakuna cha ziada alichofanya kuwashawishi Waingereza wamkumbuke kama
mmoja wa mashujaa wa timu ya taifa ya uingereza.Hiyo ndio sura ya pili ya Frank
Lampard,Ni tofauti na ile sura yake ya kwanza ya ushujaa,sura yake hii ya pili
imekuwa kalaha kwa waingereza.
Jamie
Redknapp,Mchezaji wa zamani wa uingereza
na mmoja wa wachambuzi bora Duniani,Yeye ni miongoni mwa watu walioumia kwa
kustaafu kwa lampard bila ya mafanikio yoyote akiwa na timu ya Taifa.Redknapp
anawatupia zaidi lawama makocha wa Lampard ,Ericksson,Cappello na Mc
Claren.Anaamini hawa ndio walisababisha kufeli kwa Lampard.Tatizo la Lampard
timu ya Taifa ilikua ni mfumo,haswa ule wa
kumlazimisha acheze na Gerald
kwenye sehemu ya kiungo.Licha ya kukosa maelewano bado Makocha hao
walikua wakiwalazimisha jambo lililopelekea tukose kuuona ubora wa Lampard
akiwa na timu ya taifa.
Huku kwetu
Tanzania yupo kiungo anayevaa sura mbili kama Frank Lampard.Huyu si mwingine
bali ni Amri Kiemba.Licha ya kuwa umri umemtupa mkono lakini bado mguu wake
unataka kucheza mpira.Licha ya damu yake kupoa lakini bado ubongo wake unafanya
kazi vizuri.Amri kiemba ni miongoni wa viungo bora kuwai kutokea nchini.Kiemba
licha ya kupata mafanikio akiwa na timu za Yanga na Simba lakini sasa
anaonekana kuchoka akiwa kwenye klabu yake ya Simba.Kiemba amekuwa si lolote si
chochote kwenye kikosi cha Patrick Phiri.Lakini Juzi wakati Taifa stars
wanacheza na Benin niliiona sura ya pili ya kiemba kwa dakika alizocheza.Mpaka
kipindi cha kwanza kinaisha alikua mmoja wachezaji wangu wa3 bora wa kipindi
hicho cha kwanza.Ukiachana na goli lake murua alilofunga alikuwa msaada mkubwa
kwenye timu haswa kwenye kuunganisha mashambulizi ya timu.Kiemba niliyemuona
dhidi ya benin amenifanya niamini kuna kiemba wawili,Kiemba wa Simba na Kiemba
wa Stars.
Nafahamu
takribani misimu miwili iliyopita timu ya simba ilijengwa kupitia kwa
kiemba.Lakini mimi namzungumzia kiemba wa msimu huu anayepewa dakika 10 mpaka
20 tu na kocha phiri.Katika mechi zote
za Simba msimu huu Amri Kiemba ametumika kama mchezaji wa akiba na hakuna hata
mechi moja aliyoingia na kuleta uhai kwenye timu ya simba.Amekuwa kiemba mwenye
kiwango kibovu kuwai kumshuhudia akiwa kwenye vilabu.Lakini niakenda mbali
nikagundua kuwa kiemba anavyotumiwa simba ni tofauti na kocha wa stars
anavyomtumia.
Kocha wa Stars amegundua kiemba wa
sasa umri umekwenda,hana pumzi wala kasi aliyokua nayo miaka mitatu
iliyopita.Alichokifanya kocha wa Stars ni kuweka watu nyuma ya kiemba wamkabie
huku yeye akiwa huru kupandisha mashambulizi.Kiemba wa stars anacheza mbele ya
Erasto nyoni na Mwinyi kazimoto huku
kazi yake ikibaki kusaidiana na
Ulimwengu kuhakikisha stars inapata ushindi.Amri kiemba wa sasa si mchezaji wa dakika
90,Mfumo wa kocha wa stars wa juzi umetufanya tuone dakika 45 bora za amri
kiemba kwa msimu huu.Kiemba wa pili ni kiemba wa simba.Kiemba wa Simba ana
majukumu mengi ambayo hayazingatii hali yake.Kiemba akiingia anapewa jukumu la
kuchezesha timu na kuhakikisha anawalisha washambuliaji wa simba na wakati huo
huo anahakikisha anakaba vyema kwenye zone(kanda) yake kuhakikisha mipira
haipiti kuelekea kwenye lango la simba.Huo ndio mfupa uliomshinda lampard akiwa
kwenye timu ya taifa.Anapewa majukumu mengi mno.Yeye mwenyewe aliwai kukiri
kuwa mfumo wa 4-4-2 wanaopenda kutumia England ndio unamfanya ashindwe
kutakata.Mfumo huo unafanya katikati ya uwanja kazi zote za kukaba na
kupandisha mashambulizi zifanywe na watu wawili ambae ni yeye na Gerald.Wakati
Chelsea anacheza na na Ramires na Matic,au Obi,City anacheza na Yaya toure na
Fernandinho au Fernando kwanini kusiwe na tofauti na timu ya taifa anapocheza
na Gerald tu?. Ubora na sura moja ya Babu Andrea pirlo unatokana na uwepo wa
Pogba na Marchisio juventus,pia uwepo wa Marchisio,Rossi na Montollivo katika
timu ya taifa ya Italia
Kiemba akiwa na Umri wa Pirlo
anahitaji msaada mkubwa ili aweze kuleta matunda kwenye timu.Simba kama inataka
Sura ya kiemba ifanane na sura yake akiwa na Taifa Stars inabidi ibadili mfumo
unaompunguzia majukumu uwanjani Amri Kiemba.Uwezi kuuona ubora wa kiemba kwenye
mfumo wa 4-4-2 wanaopenda kuutumia Simba.Juventus leo wangekua wanatumia 4-4-2 kusingekuwepo na nafasi ya pirlo
uwanjani.Kocha Phiri hana Budi
kubadilisha mfumo kama anataka kuuona ubora wa kiemba japo kwa dakika 45
tu.Kama Simba wataendelea na mfumo wao huu watarajie kuendelea kuona sura mbili
za kiemba kama ilivyokuwa kwa Super Frank Lampard.
Na allen kaijage
0655106767
kaijagejr@gmail.com