Breaking News
Loading...
Wednesday, 1 October 2014

Info Post




Bechkam, Jay Z na Beyonce walikua ni kati ya mashabiki waliohudhuria katika dimba la Parc Des Princes jijini Paris Ufaransa kushuhudia Barcelona wakipata kichapo cha bao 3-2 toka kwa wenyeji PSG katika mchezo wa kundi F wa ligi ya mabingwa Barani Ulaya.



PSG ikicheza bila ya nyota wake Zlatan Ibrahimovic iliwatumia viungo wengi wenye kasi kama nahodha Thiago Motta, Blaise Matuidi, Marco Verrati huku wakiwatumia Lucas Moura na Javier Pastore upande wa winga na mbele alisimama Edison Cavan iliweza kupata bao la kwanza kupitia kwa mlinzi ghali kabisa duniani kwa sasa David Luiz dakika ya 10 tu ya mchezo kabla ya Barcelona hawajasawazisha dakika moja baadae kupitia kwa Lionel Messi aliyefunga goli lake la 70 katika ligi ya mabingwa Ulaya akilingana na Cristiano Ronaldo katika historia ya michuano hiyo.

Marco Verrati aliwainua mashabiki wa PSG dakika chache baadae baada ya kufunga bao safi akiunganisha pasi ya Thiago Motta na mpaka mapumziko PSG walikua mbele kwa bao 2-1.

Kipindi cha pili PSG walioonekana kuwabana vilivyo Barcelona walifunga bao lao la 3 Bleise Matuidi akifanya kazi ya ziada kuunganisha mpira wa krosi ya Gregory Van Der Wiel. Kama ilivyokua kwa goli la kwanza Barcelona wakasawazisha dakika moja baadae kupitia kwa Neymar akiunganisha mpira uliopigwa na Dani Alves. Mpaka mwisho wa mchezo Barcelona walilala 3-2.

Katika mechi zingine Chelsea,Bayern Munich,Bate wote walipata ushindi katika mechi zao huku sare zikitawala katika viwanja kadhaa.

MATOKEO KWA UJUMLA KATIKA MECHI ZOTE ZA JANA

GROUP E
CSKA Moscow 0-1 Bayern Munich
{T.Mueller 22 (Penati)}

Man City 1-1 AS Roma
{Aguero 5', Totti 23'}

GROUP F
APOEL 1-1 Ajax
{Andersen 28', Manduca 31'}

PSG 3-2 Barcelona
{David Luiz 10', Messi 11', Veratti 26', Matuidi 54',Neymar 56' }

GROUP G
Schalke 04 1-1  Maribor
{ Bohar 37',Klaas Jan Huntelaar 56'}

Sporting Lisbon 0-1 Chelsea
{ Nemanja Matic }

GROUP H
BATE 2-1 Athletico Bilbao
{Polyakov 19', Karnitskiy 41', Aduriz 45'}

Shaktar 2-2 FC Porto
{Teixera 52', Adriano 85', Jackson Martinez 89',90'}