Timu ya Taifa ya England imeifunga timu ya Taifa ya Estonia bao 1 kwa nunge katika mchezo wa kusaka nafasi katika michuano ya ulaya almaarufu Euro itakayopigwa Nchini Ufaransa mwaka 2016.Shukrani za pekee zimuendee nahodha Wayne Rooney. Rooney alifunga goli hilo dakika ya 72 kwa mpira wa adhabu baada ya mabeki wa Estonia kumuangusha winga hatari Raheem Sterling karibu na eneo la hatari.
Ushindi huo umeifanya England kufikisha point 9 na magoli 8.Pointi hizo zinaiweka England kileleni mwa group E.
Bao alilofunga Wayne Rooney linamfanya afikishe mabao 43,6 nyuma ya Boby Charton anayeshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi kwenye timu ya Taifa ya England,Mabao 49.
ENGLAND YAUA,ROONEY SHUJAA,BADO 6 KUVUNJA REKODI.
Info Post