Burudani imeahamia huku karibuni Mestalla , huu ni ujumbe unaombatana na
picha kubwa ya basi linalo zongwa na washabiki wa soka huko Uhispania.
Kimepita kipindi kirefu hatujawaona hawa watu wakisakata kabumbu la
hali ya kutia hofu wapinzani wanaokutana nao. Na hawa sio wengine bali
vijana wa Valencia au "Los Che" moja ya klabu zenye mafanikio makubwa
katika ulimwengu wa soka
Kama ulikua hujui hawa jamaa wamechukua Ubingwa wa Ligi nchini Spain mara sita, Cope del rey mara 7 na makombe mengine.
Hawa jamaa ni mabingwa lakini kwa kipindi kifupi pepo mbaya aliwapitia
nakuwapa usingizi mzito nakujikuta si lolote wala si chochote ndio uwezo
wao ulififia mithili ya mtu alie kata roho. Baada ya ushindi wa goli
tatu dhidi ya mabingwa watetezi Atletico Madrid, kocha wa Atletico
Madrid Diego Simeone anasema kwa macho wana nafasi tena ya kupata nafasi
ya kucheza michuano ya ulaya kwa kua wamebadilika kuliko ilivyotegemewa
na uwoga umesahaulika.
Yes!! Yes!! kwa haraka inaweza isikuingie akilini kwamba huu si muda
muafaka wa kuipa nafasi Valencia inaweza kua kweli lakini ipe nafasi
nafsi yako juu ya hilo Valencia imekua ni timu tishio hasa baada Nuno
kuichukua naamu ilikua haina haja ya kumbakisha Pizzi haswa katika
kipindi ambacho timu haifanyi vizuri uwanjani. Baada ya kocha Nuno
kuwasili amejaribu kuirudisha hadhi ya klabu ya Valencia kwani ameleta
uhai ameifanya Valencia kucheza mpira ambao kila mtu anatamani kuona
ukichezwa haswa katika ulimwengu wa soka la ushindani.
Valencia wanacheza mpira koo yani muda wote wanahamu ya kufika ulipo na
ukikaa vibaya basi utawaachia alama tatu muhimu. Nuno katukumbusha enzi
zile za akina Silva na David villa.
Sala ya Nuno ni zaidi ya imani anasema vipaji vya uhispania havitumiki
vilivyo hasa katika mpira wenye kasi na nguvu wao wana tumia zaid nafasi
,naamu ndio kwa jicho lake kubwa na pana katika kipindi hiki ambapo
klabu inakaribia kuuzwa na huku deni likiwa linakua basi ni dhahiri
akili ya Nuno itakua inafanya kazi mara tatu zaid ya ile ya Diego
Semeone.
Jambo la kwanza kama kocha hana papara anacheza mpira wa kiushindani
zadi huku akiweka mbinu mbadala ya ushindi zaidi kwa kutumia nguvu
wakati wa kuutafuta na kuhakikisha kua kila shambulio lina madhara kwa
wapinzani. Sala ya Nuno kwa sasa ni ile ile anayo Sali Jose mourinho
akiamini kutumia zaidi wachezaji wenye uwezo katika nafasi zao hasa
katika nafasi ambazo ni roho ya timu huyu yeye ana Javi Fuego akiwa
mlinzi huku Gomes na Dani Parejo wakiwa ndio viongozi muhimu kwa sasa
hapa ndipo unaona ili kuifunga Valencia kwa sasa nilazima utembee na
dawa ya usingizi kwa viungo hawa maridadi na makini huku ukihitaji
kuwafunga mawe miguuni akina Nicolas Otamendi , Alcacer na Rodrigo
Mpaka sasa Valencia wameshinda mechi tano na kutoa droo mechi mbili sasa
kwanini tusimuage Pizzi na kumkaribisha Nuno hapa mestalla. Karibu la
liga ni maneno kutoka kwa mashabiki wa Valencia ,najaribu kutizama
Valencia zaidi hawa wamedhamilia kupata kitu haswa na kuvaa medali ina
wezekana ikawa ni fikira ya mbali lakini kwao ni zaidi ya ndoto na
anatuahidi kua ataitafuta nafasi ya kucheza michuano ya ulaya kama
mpenzi wa Valencia inawezekana isikuingie akilini kuhusu hili kwa kua
ndio kwanza mwezi umetoka. Na wao ndio kwanza kama wageni katika ligi.
Nuno anajitahidi kutuaminisha wapenda soka kua amechukua timu yenye
vipaji ambayo inaweza kufanya makubwa hasa kuondoa fikra za utawala wa
vilabu vile pendwa kwa kua nawao wanauwezo mkubwa wa kufanya yale yanayo
onekana yalimshinda Pizzi.
Nimeandika hii ili kuwa kumbusha na kuwaambia ndugu shughuri ipo huku karibuni mestalla Valencia haoo.
By lucas_tz
Lucas kifyasi (0764665151)