Breaking News
Loading...
Saturday, 18 October 2014

Info Post
  
 
Na Rob Hughes.
Imetafsiliwa na Kocha Somola
Facebook; Kocha Somola
 
LONDON-Raheem Sterling. Kwa usiku mmoja alikuwa ni kipenzi cha kombe la Ulimwengu.  Akitumiwa na timu ya taifa ya Uingereza kama winga machachali, pale Manaus, Brazil,kuwa hangaisha walinzi wa Italia kwa spidi yake kali na jinsi alivyofungua nafasi. Siku ile aliwakumbusha wa Brazil mchezaji wao zamani, Garrincha, “Kandege Kadogo,” ambaye alichezea timu ya taifa ya Brazil vizuri sana na kuchangamsha miaka 50 iliyopita.
                Miezi minne ilipita baada ya ile mechi ya kumbukumbuku aliyocheza Sterling ule usiku pale Manaus, Sterling akapotea.  Akuchagaliwa katika wachezaji 11 wa taifa walioivaa Estonia mjini Tallin. Kisa kikiwa alimwambia kocha wake anajisikia kuchoka.
                Sterling ana miaka 19.
Kukosekana kwake kwenye timu ya Taifa ya Uingereza, ambayo ilikuwa inasaka kufuzu mashindano ya kombe la Ulaya kumezua mjadala mkali kwenye mchezo, na si kwa Uingereza pekee, bali ulimwengu mzima.  Kuna wengine wanamshangaa na kusema, kakijana kadogo, kanacheza mala mbili, mala tatu kwa wiki katesemaje kamechoka?! Akajui kwa mshahala mkubwa anaolipwa watu wengine wanaweza kufia uwanjani?!
                Upande mwingine wanamtetea kwamba, majukumu ni makubwa mno kwa mtoto mdogo anayecheza mchezo wa watu wazima kwenye timu ya Liverpool na Taifa la Uingereza. Na ndiyo inamfanya achoke, kiakili na mwili(burn out).  
Lakini bado wengine wanamwagalia kwa jicho baya.  Sana pale wanaposikia mameneja wa Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza wakilumbana, kipi muhimu, kuchezea club au taifa?  Liverpool inamtegemea sana Sterling, tena zaidi baada ya kuwauuzia Barcelona, Luis Su’arez. Vile vile kumpoteza Daniel Sturridge anaeuguza nyama ya paja, alilooumia akiitumikia timu ya taifa ya Uingereza. 
                Liverpool inauitaji sana, tena sasa hivi, ufundi na uwezo wake Sterling wa kuwafungua walinzi wa timu pinzani.  Ata mwishoni wa mwaka jana, wakati Liverpool walipokuwa kwenye harakati ya kujaribu kutwaa ubingwa wa ligi, baada ya miaka 20 kupita, ilikuwa ni Sterling zaidi, kulikoni Su’arez na Sturridge, aliweyepaa matumaini ya kutwa ubingwa. 
                Liverpool walimaliza washindi wa pili mwaka jana, na Su’arez aliondoka, na Sterling alipewa kadi nyekundu, Miami-Marekani walipokuwa wakimenyana na Equador, mechi ya kupasha kabla ya kombe la ulimwengu.  Na ata hivyo, Sterling alichaguliwa kuwa ndiye mchezaji wa kutegemewa wa Uingereza, baaada ya ufundi aliyounyesha usiku ule pale Manaus, japo Uingereza ilifungwa, alikuwa ni nyota siku ile.
                Kuna tetesi kwamba Real Madrid wanamtaka.
Na kwanini wasimtake?  Hatawafuraisha kama mchezaji wa zamani wa Uingereza aliyecheza winga, Laurie Cunningham.  Cunningham alikuwa nyota wa Madrid na timu zingine alizochozea mpaka pale kifo cha ajali ya gari kilipomkuta kule kule Spain.
                Siku zijazoo karibuni, Sterling ana majukumu makubwa mawili.  Liverpool itakapomenyana na Queens Park Rangers jumapili na jumatano ijayo watapokuwa wenyeji wa Real Madrid, katika mechi ya kushindania kombe la washindi la Ulaya.
                Q.P.R ilikuwa ni timu ya kwanza kukiona kipaji cha Sterling.  Aliiingia kwenye shule yao ya  mpira(academy) akiwa na miaka 5, akitokea kwao kwa asili, Jamaica.  Alikuwa na kipaji tangia mtoto, ata yeye, Sterling, anasema alianza kufanya jithada kuelekea kuwa mchezaji wa kulipwa akiwa ana miaka 8 au 9.
                Raheem Shaquille Sterling anajielewa ana kipaji.  Anapoenda likizo Jamaica anatumia muda mwingi kuongea na rafiki yake, Usain Bolt, jamaa mwenye kasi kali ulimwenguni.  Bolt anamwonea wivu Sterling,kwani  anatamani ingewezekana wangebadilishana nafasi ata kwa sekunde tu.  Ingawa ndiyo Bolt anafanya mazoezi na ile timu nyingine, Manchester United.  Wivu wa Bolt si wa umaarufu bali upendo wa mchezo kutoka moyoni.
                Bolt ana miaka 28, ndoto zake za kucheza mpira hazitatimia, sana sana ni kufanya mazoezi na United.
                Sterling atakayetimiza miaka 20 Disemba, ndoto zake zote zinawezekana.
Ingawa kwenye michezo na maisha ni vigumu kutabiri kirahisi.  Njia ya Sterling ilionekana nyeupe toka alipoifungia Uingereza timu ya watoto wenye miaka chini ya miaka 17, kwenye kombe la ulimwengu Mexico, miaka mitatu iliyopita.  Sasa amezaa mtoto, msichana, aliyempata toka kwenye uhusiano mfupi.  Amewahi kushitakiwa mala mbili kwa makosa ya kuwafanyia vurugu wanawake, lakini akupatwa na hatia.
                Liverpool sasa wanamlinda sana jinsi anavyoishi, ndani na nje’ ya kiwanja.  Na yeye ameamua kufanya mazoezi ya ziada ili kujiongezea nguvu za kifua(kubeba vyuma).  Ingawa anasema ataki kifua kiwe kikubwa sana kwani labda bado anakua.  Anataka awe mwepesi, uwepesi utamsaidia kukwepa walinzi wanaomkaba vibaya kwa nia ya kumuumiza. 
                Mjadala wa kuchezea taifa au club siyo wa Sterling, wala si wa Liverpool, ila ni FIFA na UEFA ratiba inayojaza mechi nyingi na kusababisha miili ya  wachezaji kuchoka, kwani haiwapi muda wa kupumzika wachezaji hao nyota.
                Nyota wengine kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo hawalalamiki kwa sababu mpira ndiyo unawafanya wawe matajiri, lakini inawezekana wengi wakacheza kwa muda mfupi kutokana na kuumia.  Sterling anaonyesha dalili za kuchukua nyazifa zao, ndoto ambazo zinaotwa na mamilioni ya watoto.
                Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza sasa wanajuzana data za wachezaji, wanatumia kwa pamoja watalaamu wa mchezo na sayansi, kutunza rekodi na kupima kama mchezaji mwili wake umechoka sana.  Vile vile kwa Sterling, hata waganga wa mawazo(Pychiatrist) wa Liverpool wanapokwenda kumwangalia mazoezini, wapo tayari kuongea na mchezaji yoyote mwingine anayeitaji msaada kwenye mazoezi ya timu ya taifa.
                Wana historia wanakumbusha, Raheem Sterling ndiye mchezaji mdogo wa pili kwenye historia kuiwakilisha Liverpool, (baada ya Jack Robinson) ambaye alikuwa mchezaji wa tatu mdogo kuiwakilisha Uingereza na wengine wachezaji wadogo kiungia timu ya taifa miaka ya karibuni walikuwa ni Theo Walcott na Wayne Rooney.
                Michael Owen aliichezea timu ya Liverpool akiwa na miaka 17 na timu ya taifa lao miaka 18.  Sasa hivi Owen ni mtoaji maoni kwenye vipindi vya michezo na anakili kwamba, alifanya makosa kutohusikiliza mwili wake kwa kucheza mechi nyingi akiwa mdogo. 
Rooney, naodha wa timu ya taifa sasa, inaonyesha imeyapita majaribu hayo, kwani karibu anafikisha mechi namba 100 na timu ya taifa.
                Sterling anawasikia watalaamu wakimwambia kuhusu kukua kwa mwili wake, lakini ni yeye mwenyewe, ndiye anajua mwili wake unamwambia nini.
 


Habari hii iliandikiwa na Mwandishi Mashuhuli wa michezo, Rob Hughes wa NYTimes.com na kutafsiliwa kwa ruhusa maalum kwa ajili ya Mwaisabula Blog na Kocha Somola.  Lengo likiwa kufundisha na kuinua mpira wa Tanzania.  Ukitaka kuisoma kwa Kiingereza, “For Young Soccer Players, How Much Is Too Much?” New York Times October 14, 2014. Naomba maoni yenu wadau, sana sana kama nimekosea Lugha. Asante.