VIKOSI
TAIFA STARSMWADINI ALLY
KAPOMBE
ERASTO NYONI
AGGEY MORICE
NADIR HAROUB
OSCAR JOSHUA
KAZIMOTO
AMRI KIEMBA
HARUNA CHANONGO
MRISHO NGASA
THOMAS ULIMWENGU
BENIN
FABIEN
TASAVI
FORTUNE
NANA
OGOUCHI
JORDAN
MAMA SEUBOI
SESSGNON
MICKAEL
DJIGLA
JODEL
Taifa stars wanatumia mfumo wa 3-5-2
2' Taifa stars wameuanza mchezo kwa kasi wanapata kona cannavaro anakosa balance ya kupiga kichwa
5' Thomas Ulimwengu anakosa nafasi ya wazi baada ya Ngasa kupiga krosi
7 ' Amri kiemba anapiga shuti kali linalopita nje kidogo ya goli la benin
12'Bado tTaifa stars wanaonekana wapo vizuri zaidi ya benin.Haruna channongo na Ngasa wanaonesha uhai mkubwa
13'Benin wanamchezea vibaya ulimwengu.Nyoni anapiga faulo benin wanaokoa
14'Ngasa na Kiemba wanagongeana pasi maridadi ,mabeki wa benin wanaokoa
16'Amri kiemba anapenyeza pasi safi kwa Ngasa ,Ngasa anaangaliana na kipa wa benin lakini refa anasema ni offside
16'Goaaaaaaaaaaaaaaaaaal Cannavaro
Erasto nyoni anapiga mpira wa adhabu unaokutana moja kwa moja na kichwa cha Cannavaro na kutumbukia moja kwa moja kwenye nyavu za benin
19' Benin wanapata faulo karibu na eneo la hatari.
wanapiga lakini inakua offside
21' Almanusura benin wasawazishe lakini beki ya Taifa stars inaondoa mpira kwenye eneo lao la hatari
22'Thomas Ulimwengu anapiga shuti kali linatoka nje kidogo ya lango la benin
23'Mrisho Ngasa,Kiemba na Ulimwengu wanaelewana kweli kweli
26'Benin wanapata faulo,wanapiga taifa stars wanaokoa
26'Nahodha wa benin sessgon anapewa kadi ya njano
27'Thomas ulimwengu anapiga shuti kali kipa wa Benin anaokoa
28'Taifa stars wanapata kona,wanapiga kona nzuri lakini inaangukia kwenye vichwa vya mabeki wa benin wanaokoa
Mrisho Ngasa aanachezewa faulo baada ya kujaribu kuipenya ngome ya benin
30'Taifa stars wanashambulia ngome ya benin kama nyuki,mashuti ya kazimoto na ulimwengu yanawagonga mabeki wa benin
32' Mshambuliaji wa BeninSeibou Mama anaumia mpira unasimama kwa muda
35'Benin wanapata kona baada ya Nadir Cannavaro kuutoa mpira nje ya eneo la hatari,Wanapiga lakini wanashindwa kumfumania Mwadin Ally na kupaisha mpira nje na mpira ni goal kick
36'Sessgnon anajaribu kuipenya ngome ya stars ndani ya box lakini Aggrey Morice anakataa na kuondoa mpira kwenye eneo la hatari la stars
38'Amri kiemba anapiga shuti kali linalowababatiza mabeki wa benin na stars wanapata kona
40' goaaaaaaaaaaaaaaaaaaaal
Amri kiemba anafunga goli maridadi baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Kazimoto
43'Amri kiemba na Mwinyi kazimoto wanatakata kwelikweli kwenye kiungo cha Stars
45'Taifa stars wanacheza couneter attack nzuri hapa baada ya kapombe na Ngasaa kugongeana pasi murua lakini kapombe anakosa balance ya kufunga na Benin wanaokoa
45'Dakika 2 zimeongezwa ,Benin wanajaribu kuliandama lango la Stars lakini mabeki wa Stars chini ya Uongozi wa Nadir Haroub Cannavaro wanafanya kazi nzuri ya kulinda lango lao
45+2' Mpira ni mapumziko
TAIFA STARS 2-0 BENIN
Maoni yangu Kipindi Cha Kwanza
Mfumo huu wa kutumia mabeki wa kati watatu unaonekana kuisaidia Taifa Stars, Mfumo huu umempa nafasi Erasto Nyoni kusogea mbele kidogo.Anawakabia Vizuri Mwinyi kazimoto na Amri kiemba ambao wanakua huru kupandisha timu mbele.Mpaka sasa Taifa stars wamemiliki mpira 53% huku benin 47%.Thomas ulimwengu na Mrisho Ngasa wanaipa uhai safu ya ushambuliaji ya stars.Mpaka sasa stars wameshapiga mashuti 8 huku Ulimwengu akipiga mashuti 4 peke yake.Kati ya mashuti hayo 8 manne yamelenga goli,huo ni wastani mzuri wa mashuti yaliyolenga goli.
Kocha wa Stars inabidi Amuingize Simon Msuva mwenye kasi kama ya Ngasa ili kubalance kazi ya mchezo kwenye pande zote mbili
USHANGILIAJI
Naona kikundi maarufu cha timu ya Simba ,Mpira maendeleo al maarufu UKAWA kinashangilia timu yao ya Taifa bila kuchoka
Kipndi cha pili Kinaanza
Benin wanafanya mabadiliko ya kipa
Fabien anatoka
Allagbe anaingia
46'Sessgnon na Mama Saebou wanaanzisha mpira katikati ya uwanja
47'Benin wanajaribu kulishambulia lango la stars lakini bado wanashindwa kumsalim Kipa Mwadin Ally
49'goaaaaaaaaaaaaaaaaal
Thomas Ulimwengu anaipatia goli Taifa Stars baada ya kuunganisha pasi nzuri ya Mrisho Ngasa
51' Kunatokea kwa sintofahamu baada ya benin kufanya mabadiliko bila utaratibu
Muamuzi anawaonesha kadi ya manjano wachezaji hao wawili wa Benin Mohamed na Baraze
55' Benin wanapata kona wanashindwa kuitumia
56'Aggrey Morice anapewa kadi za manjano baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa Benin
57'Super save kutoka kwa mwadin Ally Mwadin baada,anaokoa mpira wa hatari baada ya benin kufanya shambulizi kali kutoka kwenye mpira wa faulo
59'Taifa stars wanafanya mabadiliko
Ngasa anatoka
Juma Luizio Anaingia
60'Cannavaro anapata majeruhi baada ya kugongana na mchezaji mwezake wa stars
61'Fortune anatoka
Sessi Anaingia mabadiliko mengine kwa Benin
63'Mabadiliko mengine kwa benin
Didier anaingia
Brick anatoka
64'Habari njema kwa stars Nahodha Nadir Haroub anarudi uwanjani
66'Ulimwengu anaumia anatoka nje kupatiwa huduma zaidi
67'Stars wanafanya mabadiliko
Salum abubakar anaingia
Amri kiemba anatoka
68'Kipindi cha pili Benin wanaonekana kuimarika zaidi,Wanamiliki mpira na kushambulia kuliko stars
69'Stars wanapata Kona baada ya mabeki wa benin kuokoa krosi iliyopigwa na Kapombe
70'Aggrey morice anapaisha kona kutoka kwa Erasto Nyoni
71'Goaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaal
Juma luizio anafunga goli rahisi baada ya kumalizia kazi nzito iliyofanywa na Thomas Ulimwengu
Taifa stars 4-0 Benin
74'Thomas ulimwengu anainyanyasa atakavyongome ya Benin
Stars wanapata kona Benin wanaokoa
75'Nahodha Cannavaro anatoka
Said Moradi Anaingia
77'Haruna Chanongo anatoka
Said Ndemla Anaingia
78'Juma luizio anapiga shuti kali linalotoka nje kidogo ya lango
80'Aboubakar sure boy anaonekana kutengeneza safu maridadi ya kiungo akishirikiana vyema na Kazimoto
82'Benin wanapiga shuti lakini linakwnda nje pasi na kumdhuru kipa Mwadin Ally
84'Kona baada ya stars kugongeana pasi za kispanyola
84'Ndemla anapiga kona,Benin wanaokoa
86' Stars wanafanya mabadiliko
Mcha anaingia
Ulimwengu anatoka
87'Stars wanatakata na kuliandama watakavyo lango la benin.hakika kazi nzuri kutoka kwa sure boy,Ndemla na Kazimoto inawatoa jasho vijana wa benin
90'Kinachofanywa na ndemla na sure boy ni udharirishaji,wanapiga pasi 11 bila wachezaji wa benin kugusa mpira
Dakika 4 zimeongezwa
goaaaaaaaaal
90+2'Benin wanapata goli la kufutia machozi
mshambuliaji fadel anafumua shuti kali linalompita kipa mwadin ally mwadin
90+4' Mpira umekwishaaaaaaaa
TAIFA STARS 4-1 BENIN
LIVE....TAIFA STARS Vs BENIN
Info Post