“Kazi ya pamoja(Teamwork) inaleta matokeo mazuri, lakini maono hayo huwa ndoto pale kiongozi anapokuwa na malengo makubwa huku akiwa na timu isiyostahiki”.Najaribu kumuelewa John C Maxwell,Mchungaji maarufu na miongoni mwa watunzi bora wa vitabu Marekani.Siku zote matokeo bora huletwa na timu bora.Na timu bora ni ile inayofanya kazi kwa pamoja(teamwork).lakini ili upate timu inayocheza kwa pamoja na kwa umoja lazima utengeneze kitu kinachoitwa ‘Chemistry’(kemia)
.
Kwenye soka tumekuwa tukitumia maneno kama chemistry(kemia) huku wengi tukiwa hatujui maana yake.nilishawai kutoa maana ya chemistry wakati naizungumzia Manchester ya van gaal.Nilisema “kemia ni masomo ya atomi na mkusanyo wa atomi kuwa molyekuli.Yaani hizo atomi ukizichanganya utapata kitu kizima kinachoitwa molyekuli. ukichanganya hydrogen na oxygen unapata maji,ukichukua sodium na chlorine unapata chumvi na ukitaka kupata chumvi na maji kwa pamoja ni lazima uchanganye acid na base Mchezaji ndio atomi yenyewe na timu ndio molyekuli.
Kitendo cha kuwaunganisha wachezaji katika timu moja na
wachezaji hao kuungana katika mfumo husika ndio tunaita
chemistry(kemia).Kocha anaposhindwa kupata wachezaji husika kwenye mfumo
husika hapo ndipo tunasema kashindwa kutengeneza chemistry kwenye
timu.Na kushindwa kupata ‘chemistry’ kwenye timu ndiko kunakofanya timu
isicheze kwa maelewano na hapo ndipo tunapokosa teamwork”.
Na hili ndio tatizo kubwa linaloikabili
Simba.’Chemistry’ ndio inafanya simba isicheze kwa maelewano.Mechi
iliyopita Dhidi ya stand united kikosi cha simba kwenye sehemu ya ulinzi
kulikua na wachezaji watano ambao hawajai cheza mechi kwa
pamoja,Kiufupi wachezaji wote watano huu ndio msimu wao wa kwanza
kucheza simba kwenye ligi kuu,Ukiachana na kipa ‘Cassilas’,Mohamed
Hussein,Mugeveke,Isihaka na Miraji ndio ilikua mechi yao ya kwanza
kucheza kwa pamoja.Licha ya umri mdogo na kukosa uzoefu kwenye ligi bado
mawasiliano yalikua tatizo kubwa kwao,Utaona kabisa atomi hizi
zilishindwa kutengeneza molekyuli ya kueleweka.
Kama uliwaangalia vizuri kila mtu alikua akicheza anavyojua
yeye na si kama timu inavyotakiwa icheze,Tatizo hili lilionekana haswa
kwa mabeki wa kati,nawazungumzia Mugeveke na Isihaka.Kama Stand united
wangekua na mshambuliaji anayejua kulazimisha mashambulizi kama Danny
Mrwanda alivyokua akifanya kwenye mechi dhidi ya Simba basi bila shaka
Stand united wangeondoka na ushindi.
Ukiacha Safu ya ulinzi kwenye kiungo pia kuna
tatizo hilo hilo la kukosa muunganiko au maelewano kwa lugha
nyepesi.Kwizera,Mkude na kisiga ni miongoni wa viungo bora kabisa kwenye
ligi kuu Tanzania.Kama ni vipaji hakika Mungu amewapa ,lakini mpaka
sasa hawa watu wameshindwa kucheza pamoja kama timu.Kwizera,Kisiga na
Mkude ndio mara yao ya kwanza kucheza kwa pamoja kwenye timu moja.Kwa
haraka utagundua vipaji hivi maridhawa vimekosa kitu kinachoitwa
“Chemistry”.
Nikimuangalia Emmanuel Okwi uwanjani
namkumbuka Michael Jordan,Michael Jordan ambaye inasemekana ni mchezaji
bora wa kikapu kuwai kutokea ulimwenguni,Jordan kila timu anayoichezea
macho yote walikua wakimuangalia yeye.Jordan alikuwa akijitahidi kwa
hali na mali timu ishinde lakini mara nyingine timu anayoichezea inapata
matokeo mabaya yanayopelekea kukosa kombe.
Jordan alikua akiumia sana na siku moja ilibidi avunje
ukimya na akasema maneno haya “Kipaji kinaweza kushinda mechi,lakini
akili na kufanya kazi kwa pamoja ndipo kunashinda kombe”.Ukiangalia
jitihada anazofanya okwi uwanjani ni kama wamemsusia timu.Hapati
ushirikiano unaohitajika kutoka kwa wachezaji wenzake,Mpaka sasa Simba
imefunga magoli 4 hakuna hata goli moja lisilomuhusisha Okwi.Lakini
ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua washambuliaji wa simba wamekosa
‘combination’,Hapo ndipo tunarudi kule kule kwenye “Chemistry”
Kabla ya msimu huu kuanza simba ilitema
wachezaji zaidi ya 11,Wachezaji 11 ni wengi sana,ni sawa na kikosi
kamili uwanjani.Ukichukua maamuzi magumu ya kutema wachezaji 11 kwenye
timu kwa msimu mmoja maana yake unataka kujenga timu upya.Simba wana
wachezaji wengi wapya ,pia wana kocha mpya,Japo inawezekana lakini si
rahisi kwao kupata kombe kwa msimu huu huku wakiwa na kila kitu
kipya,Kipa na mabeki wageni,Viungo na washambuliaji wapya.
Simba chini ya kocha Phiri inabidi wapewe muda
wa kujenga timu imara ya misimu ijayo,Kupata “Chemistry” kwenye timu
kunahitaji muda wa kutosha.Simba inabidi impe uhuru kocha Phiri msimu
mzima ,huku wakimuhakikishia kibarua chake ili afanye kazi ya kujenga
timu bila presha yeyote.Wapenzi na wadau simba inabidi wakubali
kuupoteza msimu huu kwa ajili ya misimu bora ijayo.Simba kwa kikosi
hichi walichonacho kina wachezaji wengi sana wenye vipaji.Nafikiri baada
ya msimu huu Simba watakua wameshapata “chemistry” ,nafikiri phiri
atakua ameshachanganya atomi zake vizuri na kupata molekyuli imara.Nina
imani Simba wakifanya hivi watarudi tena kama timu ya kuogopwa Afrika
mashariki na kati.
Na allen kaijage
kaijagejr@gmail.com
0655106767
Na allen kaijage
kaijagejr@gmail.com
0655106767