Klabu ya Arsenal inapanga kutoa kitita cha £8m ili
kumsajili mlinzi wa kati wa klabu ya Celtic ya Scotland Muholanzi Virgil
van Dijk mwezi januari.
Klabu ya Arsenal imefanikiwa kuipiku klabu ya Chelsea na
kukalia kiti cha uongozi katika mbio za kumnasa mshambuliaji hatari wa
klabu ya Benfica Mbrazil Anderson Talisca mwenye thamani ya £17m.
Klabu ya Aston Villa inapanga kumpa mkataba mpya kiungo
wake kinda Jack Grealish ili kuzima jaribio la klabu ya Chelsea
kumsajili mwezi januari.
Klabu ya Real Madrid imeongeza mbio za kumuwania mlinda
mlango asiye na furaha katika klabu ya Chelsea Peter Cech (31) ili
kujiimarisha katika mbio za kuusaka ubingwa wa ligi ya La Liga.
Mshambuliaji wa klabu ya Westham Muingereza Andy Carroll
amesema hana mpango wa kurudi katika klabu yake ya zamani ya Newcastle
hivi karibuni licha ya kutokuwa na namba ya kudumu katika klabu hiyo ya
London