Miamba ya soka nchini Tanzania Simba na Yanga inatarajia
kukutana leo kuanzia majira ya saa kumi jion ktk uwanja wa taifa,huku
joto la mpambano huu likiwa zaidi ya asilimia 90
Kama ilivyo ada kwa timu hizi zinapokutana , tayari hisia za uchawi zikiwa zinatawala ili kutafuta ushindi,
kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma. Mara nyingi viongozi wa timu hizi hukanusha tuhuma za kujihusiha na uchawi kwa kudai kuwa ni uvumu na uzushi ambao upande mwingine wa upinzani huutoa ili kuweka akiba kuwa kama watafungwa basi ni kwa njia ya giza.Kwa kipindi hiki , nazi huwa adimu na silaha kubwa za kuumiza upande mwingine huku njiwa wakirushwa na hirizi kufukiwa sehemu za magoli .Usishangae utaratibu wa kuingia uwanjani, si ajabu kuvunjwa , kwa wachezaji kutokea katika majukwaa ya mashabiki , tena kwa
mafungu.Ni mchezo wenye matukio mengi sana zaidi ya hayo nje na ndan ya uwanja,jambo la msingi tusubiri dakika 90 tuone nani ataibuka mshindi.

.....By King....