Breaking News
Loading...
Monday, 11 April 2016

Info Post

Michuano ya kombe la FA leo kati ya Simba na Coastal Union ya Tanga umeisha kwa timu kongwe na iliyotegemewa kuibuka kidedea ya Simba Sports kuangukia pua kwa kufungwa magoli 2-1.
Coastal inakamilisha idadi ya timu 4 zilizopenya katika ngazi ya nusu fainal ikitanguliwa na Yanga, Mwadui na Azam na hivyo kusubiri droo ya kesho.
Yusuph Sabo ndiye aliyepeleka msiba kwa kufunga magoli yote mawili na lile la Simba likifungwa na Hamis Kiiza.
Simba iliingia uwanjani ikijiamini mno kuwa ni lazima itatoka na ushindi hasa ukiangalia kuwa wapinzani wao ni wa mwisho katika ligi ya Vodacom, lakini walisahau kuwa timu yao haikuwa na mazoezi ya kutosha baada ya kupumzika kucheza mechi na kupunguza uzito wa mazoezi, hicho ndio kitu pekee kilichowatoa Simba ingawa mengi yatasemwa.
Coastal ilijiandaa kwa vita huku ikiwa imerudisha wakongwe wake kama kina Razack Yusuph Careca kuongeza nguvu kwa kocha wao Ally Jangalu hivyo walijiandaa vizuri na pambano hilo na ndio siri ya ushindi