Breaking News
Loading...
Monday, 30 April 2018

Info Post



Ushindi wa Spurs wa  2-0 dhidi ya Watford unaendelea kuongeza mshikemshike ya nani atashinda nafasi ya nne ambayo hivi sasa imeshikiliwa na Liverpool wenye pointi 72 huku wakiwa wamecheza michezo 36. 
Spurs wanafikisha pointi 71 pungufu ya alama moja tu ya zile za Liverpool na wakiwa wamecheza michezo 35 pungufu ya mchezo mmoja.

Katika mchezo huo Mchezaji nyota wa timu ya Tottenham Hotspur Harry Kane alikuwa anacheza mchezo wake wa 150 wa ligi kuu akifikisha idadi ya magoli 105, na ni Alan Shearer pekee aliyefunga magoli zaidi 121 katika mechi 150 , magoli ya Spurs yalifungwa na Harry Kane pamoja na Dele Alli.