Yanga Sc ya jijini Dar es Salaam imeifunga Magoli 2-0 klabu ya Welayta Dicha ya Ethiopia katika kombe la shirikisho Afrika.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Rafael Daudi dakika ya kwanza ya mchezo na msumari wa mwisho wa kuwateketeza Dicha ukiwekwa Nyavuni na Emmanuel Martin Dakika ya 54.
Dicha itawabidi washinde magoli 3+ katika mchezo wa marudiano ili waweze kusonga mbele katika mashindano hayo.