Gianluigi Buffon ametangaza kwamba ataondoka Juventus mwishoni mwa msimu huu baada ya miaka 17 ndani ya klabu hiyo.
Mabingwa wa Serie A wanawakaribisha Verona jijini Turin siku ya jumamosi mechi ambayo itakuwa ya mwisho kwa Buffon mwenye umri wa miaka 40 ndani ya Juventus.
Buffon ameiongoza Juventus kama nahodha kwenye kutwaa taji la saba mfululizo la Serie A na taji la Copa Italia mara nne mfululizo.
. " Jumamosi itakuwa mechi yangu ya mwisho ndani ya Juventus . Nafikiri ni njia sahihi ya kumaliza safari hii nzuri ."
. " kwa sasa najua kwamba jumamosi nitacheza mechi. Siku chache zilizopita ilikuwa uhakika kwamba nitaacha kucheza soka. Lakini sasa hivi kuna mapendekezo mazuri mezani kwangu."
Katika muda wake ndani ya Turin, Buffon amevunja rekodi nyingi, zikiwemo za kucheza dakika 974 bila kuruhusu goli , akipata jumla ya ' Clean Sheets ' 294 na kutwaa mataji 9 ya Serie A.