SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya 'UEFA', limemteua rasmi mwamuzi ambae atacheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hapo kesho mjini Kiev.
UEFA imemchagua mwamuzi 'Milorad Mazic' kutoka Serbia, ambaye yeye ndiye atasimamia sheria 17 za soka katika fainali hiyo.
Mazic ni mzoefu mkubwa sana katika mechi za Ulaya na amekuwa na uzoefu tangu mwaka 2009. Tayari katika msimu huu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ameshachezesha mechi nne.
Mwamuzi huyo mwenye miaka 45, pia ameshachezesha fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 pamoja na michuano ya UEFA EURO mwaka 2016.