klabu ya Simba SC Imefanikiwa Kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano ya SportPesa Super Cup huko Kenya Baada ya Kupata Ushindi Hii Leo.
Katika Mchezo wa Leo Simba SC Ilikuwa Inacheza Na Kariobangi Sharks na Mpaka Dakika 90 zinamalizika hakuna timu iliyoona Mlango wa Mwenzake na Kuamuliwa kwa Mikwaju ya Penati.
Katika Changamoto ya Mikwaju ya Penati Simba SC Imetinga Kwa Kufunga Penati 3 Dhidi ya 2 za Kariobangi Sharks...Shujaa wa Mchezo ni Mlinda Mlango wa Simba Aishi Manula Ambaye Kaokoa Penati Mbili.
Pia Klabu ya Simba Inakuwa Klabu ya Kwanza kutoka Tanzania Kufuzu Baada ya hapo Jana Yanga na JKU kutolewa na Timu ya Tatu Kati ya Timu zilizofuzu Nusu Fainali Sasa Imeunga na Gor Mahia na Kakamega Home Boys.
Wengine ni Singida United kujiuluza hapo Kesho Mbele ya Miamba Wengine wa Kenya AFC Leopards.
Kariobangi Sharks 0-0 Simba SC
Penati 2-3