Haji Manara na msemaji wa Simba SC ameshinda tuzo ya mhamasishaji bora wa mwaka katika klabu hiyo.
Golikipa Aishi Manula ameshinda tuzo ya golikipa bora wa mwaka wa Simba SC.
Mshambuliaji wa Simba SC na mganda Emanuel Okwi ameshinda tuzo ya mshambuliaji bora wa mwaka wa Simba SC.
Seleman Matola ameshinda tuzo ya heshima ya klabu ya Simba SC 2018.
Emmanuel okwi ndio mshindi wa tuzo ya mshambuliaji bora wa Simba SC msimu wa 2017/2018
Shiza Kichuya ametangazwa mshindi wa tuzo ya kiungo bora wa Simba SC msimu wa 2017/2018
Golikipa Aishi Manula ndio ametangazwa mshindi wa tuzo ya golikipa bora wa msimu wa Simba 2017/2018
Msanii MwanaFA ameshinda tuzo ya muhamasishaji bora wa Simba SC kwenye mtandao 2017/2018
Tuzo ya shabiki bora imeenda kwa marehemu Fihi Kambi ambaye amepokelewa na mtoto wake kwa niaba
John Raphael Bocco ndio ameshinda tuzo ya goli bora la mwaka la Simba SC msimu wa 2017/2018
Kaimu Rais wa klabu ya Simba, Salim Abdalla "Try Again" ametwaa tuzo ya kiongozi bora wa mwaka wa klabu ya Simba
Tawi la Klabu ya Simba "Ubungo Terminal", limetajwa kuwa tawi bora la Klabu ya Simba
John Bocco ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Simba SC msimu wa 2017/2018 hii ni tuzo ya pili ya Bocco usiku wa leo
Tuzo ya benchi la ufundi imekwenda kwa viongozi wote wa benchi la ufundi la ufundi la klabu ya Simba