Wakati Manchester utd wakiwa tayari kupeleka ofa kwa Atletico Madrid kumchukua kiungo Arda Turan, Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers
amesema hana mpango wa kumchukua Mario Balotelli kutoka AC Milan, baada
ya mchezaji huyo kuhusishwa na Anfield (Daily Mirror), Manchester City
wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa Porto Eliaquim Mangala, 23,
kwa pauni milioni 32 (Manchester Evening News), Tottenham wapo karibu
kufikia makubaliano na Villareal kumsajili beki wa kati Mateo Musacchio,
23, (Times), meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kuwapa
Southampton winga Nacer Chadli ili kuwashawishi kumchukua Morgan
Schneiderlin (Sun), meneja wa West Ham Sam Allardyce anataka kumchukua
winga wa Manchester United, Wilfried Zaha, 21 (Sun), West ham pia
wanamtaka Peter Crouch, 33, kutoka Stoke City kuziba pengo la Andy
Carroll ambaye ni majeruhi (Daily Express), meneja wa Southampton,
Ronald Koeman anataka kumsajili winga chipukizi wa Manchester United
Demetri Mitchell kwa mkopo (Daily Mirror), AC Milan wanamtaka kipa wa
Liverpool Pepe Reina, lakini kipa huyo anataka mshahara mkubwa (Daily
Mail), meneja wa Crystal Palace, Tony Pulis anamyatia beki wa Stoke Marc
Wilson (Daiky Star), Newcastle wana matumaini ya kumsajili beki wa kati
kutoka Nottingham Forest Jamaal Lascelles, 20, kwa pauni milioni 3
(Daily Mirror), Tottenham wanafikiria kumchukua Samuel Eto'o, 33, baada
ya kuondoka Chelsea (Tuttosport), Liverpool wanakaribia kumsajili
Alberto Moreno, 22 kutoka Sevilla kwa pauni milioni 16 (AS), kiungo
Marco Reus, 25 ambaye amehusishwa na kwenda Bayern Munich na Liverpool
atabakia Borussia Dortmund kwa msimu mwingine (L'Equipe), mkataba wa
pauni milioni 60 kati ya Real Madrid na Paris St-Germain juu ya winga
kutoka Argentina Angel Di Maria huenda ukakamilika katika siku mbili
zijazo (Marca), Liverpool imetoa dau la pauni milioni 5 kutaka kumsajili
beki wa Barcelona Dani Alves, 31 (Mundodeportivo), Wolfsburg
wanamtazama mshambuliaji wa Chelsea Fernando Torres, 30, baada ya
kushindwa kumchukua Romelu Lukaku, 21 aliyekwenda Everton (Bild), Real
Madrid wanataka kumchukua kiungo wa Wolfsburg Luiz Gustavo, 27 iwapo
Sami Khedira ataondoka. Arsenal na Chelsea wanamfuatilia kiungo huyo
(Bild), beki wa kati kutoka Brazil, Miranda amekataa kwenda Cheslea,
Manchester United na Barcelona, na badala yake atasalia Atlètico Madrid
(Marca), Juventus wanaonekana kukata tamaa ya kumzuia Arturo Vidal baada
ya Manchester United kutoa pauni milioni 40. Mabingwa hao wa Italia
watamtaka Nani na Javier Hernandez katika mkataba huo (Corriere dello
Sport). Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho
tukijaaliwa. Uwe na siku njema- Cheers!!!..(E.L)