Hakuna anayeweza kupingana na mimi
kwamba pesa ndio kila kitu, wengine wameshakuwa na misemo mingi sana wakiinadi
pesa wakiitambuliha pesa utasikia wengine wakisema pesa ni sabuni ya roho sasa
naamini wote ni wasafi na hata wachafu waajua nini maana na umuhimu wa sabuni
katika maisha ya kila siku juu ya hili sina shaka kabisa na nina uhakika na imani
zenu. Kila mtu anapogeuza shingo kutazama mashariki na magharibi, kaskazini na
kusini huwa wanaangalia pesa na kuiwaza pesa katika akili zao. Hilo sio kwa
watanzania tu bali kwa watu wote na duniani kote kwasababu hili ndilo suluhisho
na njia kuu ya mawasiliano duniani. Huku kwetu tukiziita shilingi na wenzetu
wanje wakiziita “dollar” au “paund”.
Huwa nawakumbuka sana wana harakati
wengi, wengine wakidai uhuru wengine wakidai Amani au mabadiliko katika nchi
zao. Tusiende mbali sana hapa kwetu Tanzania alikuwepo mwana harakati mmoja
ambaye alikuwa mwalimu wa mababu zetu na baadaye kuwa kiongozi wetu nadhani
wote wanamfahamu Mwalimu Julius Nyerere na sitaki kuzungumza mengi kuhusu baba
yetu wa taifa lakini naamini hakutumia pesa kama sabuni ya roho kushinda na
kupata uhuru bali alitumia mikakati mikubwa sana na akili nyingi kupata hayo,
hakuwa mwingi wa maneno bali mwingi sana wa matendo na hatua. Naamini na najua
bila yeye na mikakati yake usingekuwa mahala tulivu penye kivuli ukipata
kinywaji baridi na kuisoma hii makala.
Sasa imefika watu wawaze maendeleo
sana sana kuliko pesa. Ni kweli pesa ni sabuni ya roho lakini hutumika kuleta
maendeleo au kubomoa kabisa maendelo katika jamii. Naamini juu ya hili tunayo
mifano mingi sana kwani tunaona wenye pesa na walo na maendeleo na wenye pesa
lakini hawana maendeleo sasa ni jukumu lako na uamuzi wako kuchagua upande
unaokufaa wewe katika maisha yako.
TFF, hiki ndicho chama
kinachoshughulikia maswala yote ya mpira wa miguu ya hapa nchini kwetu Tanzania
na kushika hisani ya chama kikubwa duniani cha FIFA katika taifa letu hili.
Uongozi mzuri ni kitu nasaha na chenye mashiko makubwa sana katika muendelezo
wa chama hichi ili kiweze kuyanyua mpira wa Tanzania ambao upo katiaka kiwango
cha chini sana katika viwango vya FIFA. Mabadilko makubwa sana yanahitajika kwa
ajili ya kunyanyua kiwango cha mpira kama ambavyo viongozi wa serikali yetu
wanahangaika kuyanyua viwango vya elimu.
Nafahamu wazi kuwa nchi yetu ina
uchumi mdogo sana japo si masikini. Na pia naamini katika kila bajeti ya mwaka
kuna fungu linatengwa kwa ajili michezo mbalimbali mmojawapo ukiwa ni mpira wa
miguu ambao ndio una mashabiki wengi kuliko michezo mingine hapa nchini kwetu.
Kwa hili nashawashika sana kuamini na kuona kwamba kila mwaka lipo fungu kwa
ajli ya Tff. Na fungu hili si kingine bali ni pesa ambayo wengine wanaiita
sabuni ya roho ambayo sijui ni kiasi gani lakini naamini inatosha kwa kiasi
chake kusogeza hata hatua tatu au nne za mpira wetu hasa ligi yetu ya nyumbani
yani Ligi kuu ya Vodacom.
Najua unaweza kujiuliza maswali
mengi ambayo hata mimi najiuliza kwamba hizi pesa kila mwaka huwa zinaenda
wapi. Hilo mimi na wewe hatulifahamu lakini naamini pesa inatumika bila
mikakati maalumu na hivyo kubakia kubeba jina la sabuni ya roho peke yake na
siyo pesa kama chazo cha maendeleo. Hivi hawaoni jinsi ambavyo wenzetu wanavyoambatanisha pesa
na mikakati thabiti kabisa juu ya swala hili. Zipo nchi nyingi ambazo ni
maskini kuliko sisi lakini wana maendeleo ya kisoka kuliko sisi, unafikiri
kwanini, yote haya yanawezekana kama
viongozi wa Tff watapunguza mahojiano na kuamua kuthubutu kufanya
mikakati na matendo ili kuboresha na kuweka misingi bora ya soka.
Imefika wakati Jamali Malinzi na
kamati yake yote waamue kutuonesha mambo mapya na mazuri, nataka na natamani
katika uongozi huu mpya wa Tff ipo siku moja ntamchukua rafiki yangu Jerrylove
au Allen wanipeleke nikashangae vipaji lukuki ambavyo vitakua vikiiandaliwa
katika shule ndogo za mpira “Football Academy” au tutakwenda kushuhudia Simba
au Yanga zikicheza mpira katika viwanja vyao wao wenyewe vya nyumbani na siyo
uwanja wa taifa kama ilivyo Azam Fc pale Chamazi. Naamini mimi na wewe na hao
rafiki zagu tutafurahi sana. Ni kweli pesa ni kila kitu lakini kama haina na
haijawekewa mikakati endelevu basi pesa itabaki kuitwa sabuni ya roho na ni
dhahiri itashindwa kabisa kuleta maendeleo na kunyanyua mpira. Naamini
mwenyekiti wa Tff na viongozi wake wataitumia pesa kurudisha morali na muamko
wa mpira na kuiweka ligi yetu katika hadhi ya kimataifa ili mimi na wewe
shabiki mwenzangu tuweze kuingia katika historia ya moja ya watu kuwahi
kushuhudia ligi bora na vipaji vya ajabu kama ilivyo kwa waajentina
wanavyojivunia Messi na Maradonna.
Na,
Kelvin
Kiimbila Jr,
0719580495,