Wachezaji wa arsenal Aaron Ramsey, Jack Wilshere na Mikel Arteta
wataikosa mechi ya Galatasaray baada ya kocha arsenal wenger kuthibitisha watakua nje wiki
ijayo- maana yake majeruhi hao wataukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi
ya Galatasaray unaotarajiwa kuchezwa Jumatano
Pia wachezaji hao wapo kwenye hati
hati ya kuukosa mchezo wa Ligi Kuu ya
England dhidi ya mahasimu wao wa jiji la londonChelsea Jumapili ijayo,
wachezaji hao wote walipata majeraha jana katika sare ya 1-1 na Tottenham
Hotspur Uwanja wa Emirates.
Wenger amesema: "Sifahamua muda
mrefu kiasi watakuwa nje, lakini watakosekana wiki ijayo. Nafikiri Ramsey ni
nyama (maumivu), na Arteta ni misuli ya nyuma ya mguu. Wilshere ni kifundo cha
mguu,".