Breaking News
Loading...
Sunday, 28 September 2014

Info Post


Yanga SC vijana wa Jangwani wamezinduka na kuitandika Prisons ya Mbeya kwa 2-1 katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom uliomalizika jioni hii katika uwanja wa Taifa Jijini.

Ikiwa na Kumbukumbu mbaya Ya kufungwa na Mtibwa katika mechi ya ufunguzi Yanga iliingiza "silaha" zake zote wakiwemo Wabrazil Jaja na Continho na kuweza kuutawala vilivyo mchezo huo hasa kipindi cha kwanza. Huku Continho akitangulia kuipatia Yanga bao kwa shuti kali la mpira wa adhabu ndogo uliopita ukuta wa Prison na kumshinda kipa wa timu hiyo na kujaa wavuni.
Hivyo mpaka mapumziko Yanga walikua mbele kwa bao hilo moja huku mchezaji mmoja wa Prison akitolewa kwa kadi nyekundu kufatia kumfanyia madhambi Ngasa.



Kipindi cha pili Prisons ambao mchezo uliopita walishinda Ruvu Shooting pale Mabatini Pwani walionekana wako vizuri zaidi licha ya kuwa pungufu na kuweza kusawazisha bao dakika ya 67 kufatia mpira wa krosi uliomkuta mfungaji wa bao hilo Ibrahim Hassan lakini Yanga walisawazisha dakika moja baadae kupitia kwa Simon Msuva ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Continho.

 Andrey Coutinho akishangilia bao lake leo dhidi ya Prisons


VIKOSI;
kosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Edrwad Charles, Kevin Yondan/Rajab Zahir dk77, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga/Hamisi Thabit dk54, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho/Simon Msuva dk58.   
Prisons; Mohamed Omar, Salum Lameya, Laurian Mpalile/Boniface Hau dk74, Nurdin Chona, Lugano Mwangama, Jumanne Elfadhil, Meshack Olest/Julius kwangwa dk35, Freddy Dungu, Jacob Mwakalobo, Amin Omary/Ibrahim Kahaka dk53 na Jeremiah Juma.