Breaking News
Loading...
Thursday, 4 September 2014

Info Post




 Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa kwenye hoteli ya Tansoma Mnazi Mmoja wakisubiri usafiri wa awamu ya pili kuwapeleka mazoezini Gymkhana.
 
Akizungumza na MWAISABULA BLOGU mmoja wa wachezaji wa Taifa Stars kwa sharti la kutoandikwa jina lake alisema kuwa tangu walivyoanza mazoezi na timu hiyo ya taifa tatizo kubwa linalowasumbua ni kukosena kwa usafiri wa uhakika kiasi kinachowapelekea kuchelewa kufika mazoezini.

“ usafiri umekuwa tatizo kubwa kwenye timu ya taifa toka tumeanza mazoezi usafiri kwetu umekuwa changamoto kwetu maana unatuchelewesha kwenye mazoezi  tumekuwa tukitumia gari dogo ‘Hiace’  ambayo uwezo wake ni mdogo kubeba wachezaji wote, inabidi irudie mara mbili kitu ambacho kinafanya tuchelewa kuanza mazoezi”. Alisema mchezaji huyo 


Timu hiyo ambayo kwa sasa inafanya mazoezi yake katika viwanja vya Gymkhana( Posta) kabla ya kusafiri mjini Bujumbura Burundi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) September 7.

Kikosi kamili alichoteua kocha Mholanzi, Mart Nooij kwa ajili ya mchezo huo ni makipa; Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga SC), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Luizio (ZESCO, Zambia).
 mazoezi yakiendelea kwenye viwanja vya Gymkhana asubuhi leo