Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Urusi Muitaliano Fabio
Capello ameibuka na kusema nyota wa Barcelona Lionel Messi ni dhaidi ya
mpinzani wake Cristian Ronaldo kwakuwa ana vitu ambavyo nyota wengine
dunia hawana.
Capella akifanya mahojiano na gazeti la As la Urusi amesema
Messi na Ronaldo ni wachezaji wa kipekee sana lakini kuna tofauti kubwa
kati yao.
Amesema ``Namuheshimu sana Ronaldo,ni mchezaji mzuri sana
na mwenye nguvu lakini hana ufundi wa asili kama alionao Messi.Messi ni
mchezaji wa kipekee zaidi huwezi kumlinganisha na yeyote,hakabiki
kirahisi."
Pia Capello amekiri kuwa alitaka kumsajili nyota huyo kwa mkopo mwaka 2005.
Anasema ``Ilikuwa ni katika mchezo wa kombe la Gamper kati
ya timu yangu ya Juventus wakati huo na Barcelona ya Frank
Rijkaard.Nilibaki mdomo wazi baada ya Messi kuipasua kama karatasi safu
ngumu ya ulinzi ya Juventus ikiongozwa na Fabio Cannavaro.Baada ya tukio
lile nikajikuta nataka kumsajili Messi kwa mkopo wakati mchezo
ukiendelea jambo ambalo lilikuwa siyo kawaida"
``Wakati nikitafakari hilo mpira ulisimama nikamfuata
Rijkaard na kumwambia humchezeshi Messi kwakuwa una nyota watatu wa
kigeni katika kikosi chako sasa kwanini usinikopeshe kinda huyu kwa
msimu mmoja?
Rijakaard akanijibu ``Tunafanyia kazi suala la kuhakikisha
Messi anapata hadhi ya kucheza La Liga na hilo huenda likakamilika baada
ya miezi mitatu au minne hivyo hatutokupa kwa mkopo atabaki kusubiri
hapa hapa jambo hilo likamilike".