Breaking News
Loading...
Thursday, 30 October 2014

Info Post

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Nchini England wakiwa pia ni mabingwa watetezi wa kombe la Ligi (Capital One) Manchester City  usiku wa jana walivuliwa rasmi utetezi wao katika kombe la Capital one baada ya kufungwa Nyumbani bao 2-0 na Newcastle United.



Manchester City ambayo ilichezesha wakali wake wote wa kikosi cha kwanza isipokua kwa kipa Joe Hart na nahodha Vicent Kompany iliduwazwa na Newcastle United iliyotumia wachezaji wengi chipukizi.

Magoli ya Newcastle United ambayo kocha wake Allan Pawdew alikua katika shinikizo la kutimuliwa baada ya matokeo mabaya ya mwanzo wa ligi yalipatikana kila kipindi, ilipata goli la kwanza kupitia kwa Rolando Aarons kufuatia makosa ya Fernandinho dakika ya 6 tu ya mchezo.

Newcastle ambao walikua wakimtumia sana Gabriel Orbaten kupeleka mashambulizi ya kustukiza langoni mwa Man City walipata goli la pili kupitia kwa Moussa Sissoko dakika ya 76 ya mchezo akitumia juhudi binafsi kuipangua ngome ya City iliyokua ikiongozwa na Mangala.

Katika mchezo huo Man City walipata pigo baada ya David Silva na Yaya Toure kutolewa nje kwa kuumia huku ikiwa ni siku mbili kabla ya kuwakabili wapinzani wao katika ligi kuu Manchester United katika dabi ya Manchester siku ya Jumapili.

MATOKEO KATIKA MECHI ZA JANA

 ● Man City 0-2 Newcastle United
●  Totenham 2-0 Brighton
●  Stoke 3-2 Southampton