Kocha mkuu wa klabu ya Real Madrid Muitaliano Carlo
Ancelotti ameibuka na kusema ni ngumu kumziba mdomo raisi wa FIFA Sepp
Blatter.
Ancelotti ameyasema hayo baada ya mapema wiki hii raisi
huyo kuibuka na kudai kuwa Lionel Messi alipewa kimakosa tuzo ya
mchezaji bora katika fainali zilizopita za dunia nchini Brazil na badala
yake tuzo hiyo ilipaswa iende kwa mlinda mlango wa Ujerumani Manuel
Neuer.
Kauli hiyo ya Blatter imetafsiriwa na wengi kuwa ni njama
ya kumpigia kampeni kijanja Neuer badala ya Cristiano Ronaldo ambaye kwa
macho ya wengi ndiye anayetazamwa kama mshindi.
Ancelotti amesema ``Ni ngumu mno kumnyamazisha Blatter na
mara nyingi nimekuwa nikishangazwa na maneno yake.Ila katika hili
sidhani kama lina maana.Ronaldo amefanya makubwa ametwaa makombe muhimu
kama Copa del rey na ligi ya mabingwa huku akiendelea kufunga magoli
kila kukicha.Dunia nzima inajua tuzo hii tayari ina mwenyewe ambaye ni
Ronaldo"