Mshambuliaji Mario Mandzukic ameibuka na kudai kuwa
aliyekuwa kocha wake katika klabu ya Bayern Munich Pep Guardiola
alimkosea heshima.
Mandzukic ambaye kwa sasa anakipiga na klabu ya Atketico
Madrid katika mahojiano aliyofanya na kituo cha Sportske Novosti,na
mahojiano hayo kuchapichwa na gazeti maarufu la michezo la Mundo
Deportivo amesema Guardiola ndiye aliyemfanya akahama Bayern Munich
baada ya kumkosea heshima na kumuona hafai.
Mandzukic aliyejiunga na Bayern mwaka 2012 na kufanikiwa
kufunga jumla ya magoli 34 katika michezo 55 anasema ``Kabla ya kuja kwa
Guardiola maisha chini ya Jupp Heynkes yalikuwa mazuri mno na ndiyo
maana haikushangaza tulipotwaa mataji matatu"
Lakini alipokuja Pep mambo yalianza kwenda kinyume nikawa
sipangwi mara kwa mara licha ya kufanya vizuri katika nafasi chache
nilizopata.Pep hakutaka hata niwe mfungaji bora wa ligi kwani licha ya
magoli 18 niliyokuwa nimefunga bado aliendelea kunidharau na kuniweka
benchi.
Nakumbuka hata katika mchezo wa fainali ya DFB Pokal dhidi
ya Dortmund licha ya kuwa nilikuwa fiti bado Pep hakunipanga.Siwezi
kumsamehe achilia mbali kukaa naye meza moja na kunywa naye kahawa
siwezi".Alimaliza Mandzukic