Kiungo wa klabu ya West Ham Alex Song amefunguka na kusema
kuwa anafikiria kubaki katika ligi ya Epl pindi mkataba wake wa mkopo
utakapoisha mwezi mei mwakani.
Song ambaye ni miongoni mwa wachezaji wapya wa West Ham
inayonolewa na kocha Sam Allardyce ambayo kwa sasa iko katika nafasi ya
nne katika msimamo wa ligi imepoteza mchezo mmoja tu kati ya sita
aliyocheza kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Arsenal.
Song amesema ``Nadhani maisha yangu yataendelea kuwa hapa.Ndugu zangu,familia yangu wote wanafurahia kuwa hapa.
Kila mara nimekuwa nikisisitiza kuwa moyo na soka langu viko England.
Song alihama Arsenal mwaka 2012 na kufanikiwa kucheza
michezo 39 tu huku msimu uliopita akishuka dimbani mara 19 pekee baada
ya kushinda kujihakikishia namba katika kikosi cha miamba hiyo ya
Catalunya.