Mwaka 1990
alizaliwa mtoto wa ajabu huko Marekani. Matthew Stepanek,mtoto aliyewashangaza
wamarekani wengi.Stepanek aliishi miaka 13 tu Duniani.Kabla umauti kumkuta akiwa
na umri huo wa miaka 13 alishatunga Vitabu bora vitano vya mashairi.Wamarekani walikua wakimuita ‘peace advocate’(wakili wa
amani) kutokana na mashairi yake yaliolenga hasa kwenye Amani,Umoja na
Mshikamano. Mashairi yake yaliwasisimua watu wengi wakiwamo watu maarufu kama
Oprah Winfrey, Larry King.Lakini zaidi alikua Jimmy
Carter,Rais wa 39 wa marekani.Carter alidiriki kusema “katika maisha yangu yote
sijawai kumshuhudia mtu wa ajabu kama Stepanek”.Jimmy Carter alikua muumini
mkubwa wa mashairi ya Stepanek yaliyohamasisha umoja baina ya watu wa Marekani.
“Unity is strength.when there is
teamwork and collaboration,wonderful things can be achieved”.(Umoja
ni nguvu.Kila kwenye ushirikiano na kufanya kazi kwa umoja,Mambo mazuri
yanaweza kufikiwa).Hii ni moja ya kauli zake pendwa na ya kukumbukwa ya
Stepanek iliyohusu umoja.
Huo ni
Ubongo wa mtoto aliyeishi kwa miaka 13 tu lakini unashinda bongo za watu wengi
wenye umri mkubwa.Nashukuru Mungu nilikua mmoja wa watu walioshuhudia mechi ya
Simba na Prisons katika uwanja wa Sokoine.Wakati nasafiri kuelekea mbeya mpaka
naangalia dakika 90 za mechi hiyo
niligundua kuwa Simba ina tatizo moja tu la kukosa umoja.Simba imekosa hekima
aliyekuwa nayo mtoto mdogo Stepenak.Simba haina umoja kuanzia kwa
viongozi,Wanachama,Benchi la ufundi mpaka wachezaji.
Benchi la
ufundi la simba bila shaka limekosa mawasiliano mazuri.Wakati mechi ikiendelea
kuna muda niliona Phiri na msaidizi wake Matola wanapishana kauli.Napata
mashaka kama maamuzi ya kiufundi kama
yanatolewa na benchi nzima au mtu mmoja pekee.Tangu nianze kushuhudia soka sijawai
ona mabadiliko mabovu mwalimu anafanya kama aliyoyafanya phiri.Kwa kumuingiza
kiemba na kutoka kwa Ndemla pale phiri alizidiwa akili na mamilioni ya
watanzania. Kuna muda naona kabisa Phiri anafanya maaumizi bila kushirikisha
benchi lake la ufundi.Sidhani kama Matola aliridhia mabadiliko yale mabovu
yaliyofanywa na kocha phiri.Phiri anaweza kuwa kocha mzuri kuliko Matola,Lakini
Matola anawajua wachezaji wa simba vizuri kuliko Phiri.Wachezaji wengi wa simba
wamefika hapo walipo kwa nguvu za Matola.Phiri anachopaswa kufahamu kuwa
Matola ana nguvu kubwa ndani ya kikosi
cha Simba.Lakini pia kuna tetesi ndani ya timu hiyo ya kuwa kocha huyo msaidizi anahusika kuigawa timu
hiyo kupitia baadhi ya wachezaji,nilipomuuliza kocha huyo alikataa
katakata,lakini lisemwalo lipo kama halipo basi li njiani.Kitu cha msingi ni kumaliza tofauti zilizopo ndani ya benchi
la ufundi.Lazima kuwepo na umoja, ushirikiano na mawasiliano mazuri kati ya
kocha na wasaidizi wake.
Nikihama
kwenye benchi la ufundi nagundua pia wachezaji wa simba pia wamegawanyika.Kuna
siku niliandika kuhusu simba walivyokosa muunganiko ‘chemistry’.Lakini wakati wa mechi yao na Prisons nikagundua
kuna mgawanyiko zaidi ya ‘chemistry’ ndani ya timu hiyo.Nilianza kugundua tu
wakati Singano anatoka kupisha Haruna chanongo.Jicho la chanongo liliniambia
kuna kitu kinaendelea ndani ya kichwa cha Singano.Pia machozi ya Okwi na Jonas
Mkude kuna kitu yalikua yanamaanisha.Waswahili wanasema ‘ukimuona mtu mzima
analia ujue kuna jambo’.Jicho la chanongo kwa Singano,Machozi ya okwi na
mkude,Pia kujituma kwa wachezaji wachache uwanjani kunanifanya niamini kabisa kuna kitu
kinaendelea baina ya wachezaji wa simba.Niliposikia Amri kiemba amesimamishwa
Simba wala sikushangaa,Lakini bado nawaza kama Singano nae ataendelea kuwa
mchezaji wa Simba.Wachezaji wa simba waliopo wanaonekana hawapo tayari kufanya
kazi pamoja.Wachezaji hao licha ya kutoelewana ndani ya uwanja wanaonekana
hawaelewani zaidi nje ya uwanja.
Nikirudi
kwa viongozi wa simba nahisi huko ndipo matatizo yanapoanzia.Kuna viongozi
Simba wanaonekana kuwa na sauti kubwa ndani ya timu kuliko vyeo walivyo navyo.Siku
hizi yupo kiongozi ambaye anatoa taarifa
zote za simba ingawa si msemaji wa simba.Msemaji ni yeye,Mwenyekiti wa kamati
ya ufundi ni yeye na mara nyingine huvaa viatu hata vya Raisi wa klabu.Kuna
muda nafikiria nguvu ya Raisi wa simba
ndani ya timu hiyo.Nahisi kuna watu wana nguvu zaidi ya Raisi huyo wa simba.Pia
kuna taarifa nilizipata za kutokuwa na maelewano kati ya viongozi wawili wa juu
wa simba.Sasa kama baba na mama hawaelewani ndani ya nyumba watoto ndani ya
nyumba hiyo wataanzaje kuelewana?.Wachawi wakuu wa simba ni viongozi
wenyewe.Kutoelewana kwao ndio kunaleta kuhujumiana.
Kiukweli
hali ya simba si nzuri,hali hiyo inapelekea hata kuchukiana baina ya wanachama
wa matawi ya timu hiyo.Viongozi wa simba inabidi wawekane sawa na kila mmoja
ajue mipaka ya uongozi wake sambamba na kushirikiana na viongozi wengine na
kuvunja makundi yaliyopo ndani ya timu hiyo.Kuelewana kwa viongozi kutaleta
maelewano baina ya wanachama,benchi la ufundi na hata wachezaji.Biblia yangu
inaniambia hata Mungu hupendezwa na watu wanaokaa pamoja na kufanya kazi kwa
umoja.Kama viongozi hao wanaona tabu kusoma biblia yangu basi wakasome mashairi
ya umuhimu wa umoja ya Stepanek yaliyomshangaza Raisi Jimmy Carter.
Na ALLEN KAIJAGE
0655106767