Breaking News
Loading...
Saturday, 18 October 2014

Info Post

peter manyika jr
Timu za Simba na Yanga zimetoshana nguvu kwenye mchezo wa ligi kuu tanzania bara baada ya kwenda dakika 90 bila kufungana goli lolote.
Simba iliyokua na kikosi kilichosheheni chipukizi ilitawala karibu kipindi chote cha kwanza huku emmanuel okwi akionekana hatari zaidi baada ya kupiga mashuti kadhaa kwenye lango la yanga
Yanga ilitawala zaidi kipindi cha pili huku mshambuliaji mbrazil Jaja akipoteza nafasi ya kufunga goli dakika ya 77 akiwa anatizamana na kipa Manyika jr
Peter Manyika jr ndie alikua kivutio kwa watu wengi alionekana akiwa mwenye utulivu zaidi golini.
Mchezaji wangu bora wa mechi alikua Rajabu Isihaka aliyewahimili vyema washambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa na Jaja
isihaka akiwa na wachezaji wenzake wa simba wakishangilia moja ya magolo ya simba