Jana nilitabiri mechi 5,kati ya
hizo ni mechi 3 tu ambazo zilichezwa.Na katika mechi hizo 3 nilipatia mechi 2
na kukosea mechi moja ya Mbeya city dhidi ya Stand united.Siku ya leo
tutaangalia uchambuzi wa mechi mbili zilizobaki.
Simba Vs Ruvu Shooting
Timu ya simba ambayo haijashinda
mechi moja mpaka sasa itaingia uwanja wa taifa kusaka ushindi wake wa kwanza
dhidi ya Ruvu shooting.Ushindi wa simba leo utategemea zaidi viwango vya
wachezaji wao wawili tegemezi Emmanuel Okwi na Jonas Mkude.Emmanuel Okwi ambae
amehusika
katika kila goli ambalo simba wamefunga msimu huu anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya simba akishirikiana na Elius Maguri.Jonas Mkude ambaye kwa sasa ndie moyo wa simba,anatarajiwa kuunganisha vyema safu ya kiungo huku pia akisaidiana na mabeki wake kutoruhusu bao.Ruvu Shooting wataingia kwenye mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kupigwa bao 1 kwa bila na Coastal union ila kwa leo sioni kama timu hiyo itapata matokeo.

UTABIRI Simba 3 Vs 1 Ruvu Shooting
JKT Ruvu Vs Ndanda Fc
Maafande wa Jkt Ruvu wataingia
kwenye uwanja wa chamanzi wakiwa na hasira ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya
Polisi morogoro kwenye uwanja wa chamanzi.Ndanda iliyoiadabisha Azam fc kwenye
uwanja wa Nangwanda sijaona wataendelea kumtegemea nyota wake massawe kupata
pointi 3 kwenye mechi ya leo itakayopigwa kwenye uwanja wa chamanzi.
UTABIRI JKT Ruvu 1 Vs Ndanda 0 Fc