Breaking News
Loading...
Monday, 1 December 2014

Info Post


                       
           Msimu uliopita Real Madrid ya Spain ilifanikiwa kunyakuwa ubingwa wa ulaya na kombe la mfalme.Timu hiyo ilizungukwa na nyota wengi kama Ronaldo,Di maria,Alonso na wengine wengi.Lakini
msimu ulipoanza kocha wa Real Madrid Carlo Anceloti aliwauza baadhi ya nyota wake waliompa mataji msimu mmoja nyuma.Wengi hawakumuelewa lakini mimi binafsi nilimuelewa sana.Mwalimu wangu wa uchumi alishawai kunifundisha kuwa ukifanya kazi moja kwa muda mrefu ufanisi wa kazi hiyo lazima utapungua au ukitumia chombo(mashine) kufanyia kazi moja kwa muda mrefu,ubora na ufanisi wa chombo hiko unapungua kadiri unavyokitumia.Sambamba na hilo nilifundishwa kuhusu kitu kinachoitwa ‘Fatigue’(uchovu).Mfanyakazi anapofanya kazi moja kwa muda mrefu lazima ‘Fatigue’impitie.Haya yote yalikuwamo ndani ya akili ya Anceloti.Mpaka Madrid inachukua kombe la Ulaya,Di maria ndiye mchezaji aliyekuwa ametumika sana,Anceloti alifahamu fika hataweza kuuona tena ubora wa Di maria na Alonso kama wa msimu uliopita.Akaamua kuleta wachezaji wapya ndani ya kikosi chake.Ukiangalia Madrid ya msimu uliyopita na msimu huu ni tofauti kabisa,Mbinu wanazotumia msimu huu ni tofauti na walizotumia msimu uliopita.Tofauti hiyo inaletwa na wachezaji wapya kama Kroos na James Rodriguez.Na ndio maana mpaka sasa Madrid inaendelea kutesa.
         Huku kwetu kwenye ligi kuu ya Tanzania kuna Timu iliibuka msimu uliopita na kushangaza wapenzi na washabiki wa soka Nchini.Mbeya city ndio timu nnayoizungumzia.Mbeya city msimu uliopita walishika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu Vodacom.Kumbuka ndio kwanza timu hiyo ilikuwa inapanda daraja.Hakuna mtu aliyetegemea makubwa yaliyofanywa na wachezaji  wa timu hiyo ya mbeya city msimu uliopita.Licha ya ubora waliokuwa nao,ila faida nyingine ilikuwa hakuna timu iliyokuwa inajua mbinu na mfumo wa mbeya city.Mbeya city walitumia mwanya huo kusulubu timu zilizoshiriki ligi hiyo msimu uliopita.Timu zetu kongwe zilionja joto ya jiwe kutoka kwa miamba hiyo ya jijini Mbeya.Stamina,Pumzi ya kutosha pamoja na ‘chemistry’ aliyoitengeneza kocha Mwambusi ndio ilikua karata dume kwa mbeya City.Lakini mbeya city ile ile ya jana imeshindwa kutamba leo.
            Kila siku sio jumapili,Mpaka tunapozungumza hivi sasa timu ya Mbeya city inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara msimu huu.Timu ile ile na kocha yule yule je Tatizo nini?.Moja kwa moja nafikiria akili ya Kocha Mwambusi,Kocha huyo bado anaishi na kuamini kwenye jana yake huku mshale wake wa saa ya mkononi unakwenda kasi kweli kweli.Mwambusi amekosa ubongo wa Carlo Anceloti.Baada ya kumalizika kwa ligi kuu msimu uliopita Mbeya city hawajafanya usajili wa mana zaidi ya kumsajili Themi Felix.”Wachezaji hao wanatosha sasa tunaelekeza nguvu kwa timu ya pili itakayosaidia kujenga timu ya wakubwa.Tumefanya kwa mahitaji kwa sasa wachezaji wetu wengi wapo kwa hiyo hatukuona haja ya kujaza wachezaji wengi ambao hatutawatumia” hayo yalikuwa maneno ya katibu wa mbeya city akibariki maamuzi ya kocha wake Mwambusi. Kocha huyo wa mbeya city hakutaka kubadilisha kikosi chake akiamini kikosi alichonacho kitafanya maajabu tena kwenye ligi ya msimu huu  huku akisahau kitu kinachoitwa ‘Fatigue’.Kwa mchezo wa kutumia nguvu waliokuwa wanatumia mbeya city,Ilikua ngumu kuuona ubora ule ule wa Deus Kaseke,Mwagane Yeya na Paul nonga.Kwa nguvu kubwa walioitumia wachezaji hao walihitaji mfumo mpya,na wachezaji wapya watakaowapunguzia uchovu wao kwa msimu huu.Ila kwa mbinu zile zile anazotumia Kocha Mwambusi  lazima ufanisi wa wachezaji hao upungue.
          Kinachowakuta mbeya city si kigeni kwenye ulimwengu wa soka.Ukiangalia hata kwa upande wa Azam nao wanaathiriwa na kitu hiko hiko.Kavumbagu ndio tofauti kubwa ya Azam hii ya leo na ile ya jana iliyochukua ubingwa msimu uliopita.Kocha wa Azam nae ameshindwa kuwatafutia wakina Sure boy dakika za kupoza misuli yao iliyopmbana vilivo kuchukua Ubingwa wa ligi kuu msimu uliopiota.Sure boy hawezi kufanya kile alichokifanya msimu uliopita hasilani kwa kikosi  na mfumo huo huo.Ukienda mbele zaidi unaweza kujifunza pia kwa kwa Manchester City ya England.Kila msimu unaofuata kutoka msimu wanaochukua ubingwa  lazima wachemke.
            Tatizo la makocha wengi Duniani akiwemo Juma Mwambusi wanaamini sana kwenye mifumo na mbinu zao za jana zilizowapa mafanikio.Huku wakisahau kitu kinachoitwa ‘Fatigue’.Mbeya City lazima wasajili wachezaji wa haja angalau watatu ili kuleta chachu na kurudisha heshima ya mbeya city.Kocha Juma mwambusi inabidi atambue kwa nguvu walizotumia wachezaji wake msimu uliopita lazima abadilishe kikosi na mfumo ili kuwarejesha wachezaji hao mchezoni.Pia inabidi abadili mbinu zake alizokuwa anazitumia msimu uliopita kwani wapinzani wameshazigundua.Mbeya city ni lazima watumie kipindi hiki cha usajili kufanya mabadiliko ndani ya kikosi chao.Kwa kufanya hivyo watainusuru timu yao mkiani na kurudisha heshima kwa wana mbeya kwani ndani ya timu hiyo hakuna kingine zaidi ya Uchovu kwa wachezaji na kupoteza mazoea ya ushindi waliokuwa nayo msimu uliopita.

Na Allen Kaijage.
0655106767
kaijagejr@gmail.com