Simba inashuka dimbani jioni hii kuumana na Maafande wa Tanzania Prisons katika mchezo ambao pande zote mbili zimepania kuibuka na ushindi.
Kocha Mkuu wa Simba Goran Kopunovic, ameahidi kuwa vijana wake leo watapambana kufa na kupona kunusuru hali ya mambo kwenye timu hiyo ambayo imekua haina matokeo mazuri kwenye ligi kuu.
Timu ipo kwenye hali nzuri na wachezaji wangu nimeshawaambia umuhimu wa kushinda mechi hii. Tumefanyia kazi mapungufu yetu na tuna imani kubwa tutashinda na kujiweka pazuri," alisea Kopunovic.
Nae Kocha wa Tanzania Prisons David Mwamaja amesema kuwa vijana wake watapambana kikamilifu leo hii, ili kujinasua toka mkiani mwa ligi hiyo.
Alisema kuwa Simba ni timu ngumu ila vijana wake wako tayari kuishangaza timu hiyo kongwe leo jioni.
Simba vitani na Prisons
Info Post