Breaking News
Loading...
Monday, 13 April 2015

Info Post
Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe ametamba kuwa timu yake ni lazima itwae taji la Ligi Kuu msimu huu kutokana na ubora wao.

Tambwe ametoa kauli hiyo wakati ambapo Yanga imeiacha Azam FC inayotetea ubingwa wake kwa tofauti ya pointi 8.

Akizungumza na mwandishi wetu, Tambwe alisema kuwa kikosi cha Yanga hivi sasa ni moto wa kuotea mbali na hakuna timu itakayotoka salama mbele ya wakali hao wa Jangwani.

Alisema kuwa kila mchezaji wa Yanga ana hamu na ubingwa huo ambao hapo mwaka jana ulichukuliwa na Azam ambayo imeshaanza kupotea kwenye mbio za ubingwa.

"Tutachukua ubingwa hilo ni jambo lisilo na mjadala. Sisi tuko vizuri na kila mmoja anatambua hilo. Nawaomba wanayanga wajiandae kupata furaha," alisema Tambwe.

Kama Yanga itafanikiwa kuchukua ubingwa, itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tambwe kufanya hivyo tangu aje hapa nchini mwaka juzi