Magoli kutoka kwa Gabriel Jesus, Ilkay Gundogan na Raheem Sterling yametosha kuipa ushindi na pointi tatu muhimu Manchester City kwenye hatua ya mwisho ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka ya Uingereza.
City wameitungua 3-1 Spurs katika dimba la Wembley na kuiwezesha City kufikisha pointi 87, kumi na sita zaidi ya United ambao wanacheza kesho.
City wanaweza kuwa mabingwa kesho kama Man United watapoteza dhidi ya West Brom lakini kama United wakishinda basi City watakuwa mabingwa wikiendi ijayo endapo wakiwafunga Swansea City dimba la Etihad.