Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema kwamba kikosi chake kinaweza kuteleza na kuwaruhusu Manchester United kutwaa taji la Ligi kuu ya Soka ya Uingereza.
City wanahitaji pointi tano katika mechi zao sita zilizobaki ili kutwaa taji hilo kuelekea mechi yao ya usiku ya leo dhidi ya Tottenham Hotspurs
Wanasafiri kwenda Wembley huku wakiwa wameshapokea vichapo vitatu kutoka Liverpool kwa jumla ya 5-1 mechi mbili za UEFA na 3-2 dhidi ya vijana wa Jose Mourinho wikiendi iliyopita
Guardiola amegoma kukanusha kuanguka kwa kikosi chake na ametumia mifano ya soka la Hispania na Ligi ya NBA kuthibitisha kauli yake
. "Inaweza kutokea. Soka ni Hisia sana. Tunachoweza kufanya ni kujiandaa vizuri dhidi ya Tottenham na Swansea."
. " Ukifikiria kwamba tangu Novemba au Desemba tayari tulikuwa eti mabingwa. Baadhi ya wachambuzi na mashabiki ilipofika mwezi Novemba walikuwa wanasema tumeshakuwa mabingwa haiwezekani City kuangusha pointi. Katika wiki moja tumepoteza mechi tatu. Inawezea kutokea."
. " Kukabiliana na presha ya mwisho ya msimu ni nzuri kwa maendeleo yetu ya baadae . Lazima tuweze kuikabili. Kama tukishindwa kufanya hivyo na United wakatwaa Ubingwa basi tutasema tu " Hongereni " .
. "Kweli inaweza kutokea nakuhakikishia hilo. Real Madrid miaka kadhaa iliyopita walipoteza mechi sita mfululizo na kushindwa kutwaa ubingwa . Bila shaka inaweza kutokea hakuna shaka kabisa. Wachezaji wanajua hilo sina haja ya kuwaambia hilo."
.
. " Hapo nyuma haijawahi kutokea katika NBA kwenye fainali timu moja ipo nyuma kwa 3-1 na kurejea kutwaa ubingwa. Mwaka mmoja uliopita Cavaliers walitwaa kwa 4-3 dhidi ya t Golden State Warriors kwa kushinda mechi tatu mfululizo."