Hat Trick ya Lionel Messi na moja kutoka kwa Philipe Coutinho yameipa Barcelona ushindi wa 4-2 dhidi ya Deportivo na kutwaa ubingwa wa La Liga msimu wa 2018/2019.
Taji hilo linakuwa la 25 kwa Barcelona na kati ya hayo 9 wametwaa wakiwa na Lionel Messi na Andres Iniesta kikosini .
Lionel Messi sasa anazidi kujichimbi kileleni kwenye mbio za Pichichi kwa kufikisha magoli 32 ya Ligi na 43 katika mashindano yote , na katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha Ulaya kamzidi MO Salah goli moja. .
Mo Salah kabakiza mechi mbili za Ligi na Messi kabakiza mechi 4 ligi kuisha.