Breaking News
Loading...
Sunday, 29 April 2018

Info Post


Hat Trick ya Giovanni Simeone imetosha kuitungua Napoli 3-0 kutoka mikononi mwa Fiorentina na kuwaharibia mchakato wao wa kutwaa taji la Scudetto nchini Italia. ( Mtoto wa kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ndio kapeleka kilio Naples )

Baada ya jana Juventus kumtungua Inter Milan 3-2 kuongeza wigo wa Pointi kuwa tano ( 88 vs 83 ) leo Napoli walikuwa wanatazamia kuwafunga Fiorentina ili kufanya wigo kuendelea kuwa pointi 1, lakini imekuwa kinyume na wigo kuwa pointi 5 zikiwa zimebaki mechi tatu msimu kuisha.

Napoli walilazimika kucheza wachezaji 10 kwa muda wa dakika 82 baada ya beki wao wa kutumainiwa raia wa Senegal Kalidou Koulibaly kulimwa kadi nyekundu dakika ya 8 tu ya mchezo huu.