Magoli ya Paul Pogba na Marouane Fellaini yametosha kuipa Manchester United pointi tatu baada ya kuifunga Arsenal 2-1 katika dimba la Old Trafford.
Kwa ushindi huo Man United wanafikisha pointi 77 , Pointi 5 zaidi ya Liverpool wanaoshika nafasi ya tatu kwa Pointi 72 , na hivyo kuwahakikishi kumaliza nafasi nne za juu hata kama wakipoteza mechi zao zote zilizobaki, kwasababu Chelsea wanaoshika nafasi ya tano wana Pointi 66 na wakishinda mechi zao tatu watafikisha pointi 75 ambazo ni pungufu za United kwa sasa.
Sasa imebaki kujihakikishia kumaliza nafasi ya pili tu ambapo Liverpool na Spurs wanaweza kumfikia kutokana na wigo wa pointi na idadi ya mechi zilizobaki.
Arsene Wenger leo ndio mechi yake ya mwisho ya Ligi kuu ya Uingereza ndani ya dimba la Old Trafford akishindwa kupata pointi tatu kwa miaka 12 sasa tangu mara ya mwisho mwaka 2006 goli la Emmanuel Sheyi Adebayor.
Henrikh Mkhitaryan amefunga goli pekee la Arsenal na kuwa mchezaji ambaye katika msimu mmoja ameifunga United na Kuifungia goli pia . Alifunga akiwa United pia msimu huu..