Breaking News
Loading...
Friday, 27 April 2018

Info Post


Gwiji wa klabu ya Barcelona Andres Iniesta amethibitisha kwamba ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu .

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 amefanikiwa kucheza mechi 669 mpaka sasa katika misimu 16 , akitwaa mataji 31 na mataji matatu makubwa akiwa na timu ya taifa ya Hispania.
Iniesta ambaye amecheza mara 125 katika kikosi cha Hispania anatarajiwa kupanda ndege kwenda kucheza fainali za kombe la Dunia Urusi hapo baadae.
. " Ni ngumu sana kwangu mimi kukaa hapa na kusema Kwaheri wakati nimetumia maisha yangu yote nikiwa Barcelona. Kwa kiasi kikubwa jinsi nilivyo ni kwasababu ya Barcelona na La Masia - Nawashukuru sana."

Iniesta bado hajathibitisha rasmi wapi atahamia baada ya Barcelona.